DIWANI LTP LUPINGU AZIDI KUFUNGUKA ADAI ATAENDELEA KUFANYA KAZI NA MBUNGE WA CCM ,AWASHANGAA WAPINZANI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO

Filikunjombe  akiongoza  wananchi wake kushiriki maendeleo 
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizungunza na  wananchi wa kijiji  cha Ntumbati  waliojitokeza kushiriki maendeleo ya  kuchimba mashimo ya nguzo za umeme 

Diwani  wa kata ya  Lupingu John Kiowi (TLP) kushoto akifurahia kauli ya  mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe  (kulia) ya   kumtaka  kuhamia  CCM ili  kuendelea  kufanya kazi pamoja


 mbunge  wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  akishirikiana na  wananchi wake na  viongozi wa CCM kata ya Lupingu  kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda  kijiji  cha Ntumbati
Wananchi  wa kijiji  cha Ntumbati kata ya  Lupingu wakishirikiana na mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  (kushoto ) kubeba  nguzo za  umeme.Soma zaidi
Viongozi  mbali mbali  wakishiruikiana na mbunge pamoja na wananchi kusimika  nguzo ya  umeme 
 mbunge  wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  akishirikiana na  wananchi wake na  viongozi wa CCM kata ya Lupingu  kusimika  nguzo za umeme kwenda  kijiji  cha Ntumbati
Mbunge  Filikunjombe na  wananchi  wakifukia nguzo ya  umeme 
Mbunge  Filikunjombe na wananchi  wakishiriki kufyeka  miti kwa ajili ya kupata  njia ya  kupiga nguzo za umeme kwenda kijiji  cha Ntumbati 
Wanawake  wakiwa na watoto mgongoni wakijitolea  kushiriki maendeleo 
Mbunge Filikunjombe akiwapongeza  wanawake wa kijiji cha Ntumbati  ambao  walijumuika na waume zao katika kushiriki maendeleo ya kufyeka miti ili  kupata njia ya kupita umeme huku  waume zao  wakichimba mashimo na kubeba nguzo 
Filikunjombe akiwa na chombo chenye  chakula  ambacho  walimletea  wananchi hao ili baada ya kazi aweze kula 
Wanawake wa  kijiji cha Ntumbati wakiendelea kufyeka miti 
Mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe (mwenye shati la kijani)na timu yake  wakiongoka baada ya  kumaliza siku ya kwanza ya kuchimba mashimo na kubeba nguzo 
                                                        Na  matukiodaima.co.tz 
WAKATI  uchaguzi mkuu mwaka 2015 ukinukia  diwani wa  chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya  Lupingu  wilaya ya  Ludewa mkoani  Njombe  John Kiowi  amesema  kuwa hana sababu ya  kuendelea msimamo wake wa  kukumbatia itikadi za  chama chake na badala yake ataendelea kumuunga mkono mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe( CCM)katika  kuwaletea wananchi maendeleo.

” ndugu  zangu  wananchi  kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge  wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe  pia amekuwa mstali wa mbele katika  kushiriki tofauti na wana siasa  wengine ambao  muda  wote  wao ni watu wa majukwaani ila  vitendo sifuri …..nasema  Ludewa  imempata mbunge na niweke  wazi  hapa mimi  sio mpinzani mbabaishaji  kama  walivyo wengine ambao kila  kukicha  wao wanawaza kuipinga serikali na maandamano badala ya kuandamana kama hivi kuja kushirikiana na na wananchi kuleta maendeleo ...." 

Kauli  ya  diwani  huyo ilikuja  baada ya mbunge Filikunjombe na   wananchi wake kumtaka  kurejea  CCM  ili aweze  kufanya kazi kwa uhuru zaidi kuwatumikia vema wananchi wake kwa kuwa ndani ya CCM.

Akizungumza  wakati wa kumkaribisha  mbunge Filikunjombe  kushiriki   shughuli za maendeleo ya  kuchimba mashimo ya  nguzo za umeme na kusimika nguzo za umeme kutoka  kijiji cha Nindi kwenda  kijiji cha Ntumbati kata  ya Lupingu ,diwani Kiowi  alisema  kuwa kati ya  wabunge wa  CCM ambao  anawakubali na yupo  tayari  kufanya nao kazi na kusikiliza  ushauri  wao ni pamoja na Filikunjombe.

" Mheshimiwa  mbunge kwanza nataka  kukuhakikishia kuwa ni  mara  chache sana  kuna diwani wa upinzani akifanya kazi na mbunge wa  CCM kama  njia ya kutekeleza ilani ya CCM ......kwani  sisi  wapinzani ni  watu wa  kupinga  kila jambo hata kama linamanufaa kwetu wenyewe lakini  nakuhakikishia mimi kama  diwani wa TLP  hapa kata ya  Lupingu natamka  wazi kwanza  nitawakamata na  kuwachukulia hatua  wale  wote  wanaopinga maendeleo makubwa ambayo unatuletea  kata ya  Lupingu  bila  kujali ni kata ya upinzani.....ila na mimi nitamke wazi  kuwa napenda  sana kufanya kazi na  wewe" alisema diwani  huyo  bila kusema kama yupo tayari  kurejea  CCM ama  lah.

Kwani  alisema uchapakazi  wa  mbunge   huyo  unawavuta  wengi hata ambao  si wananchi  wa  jimbo la Ludewa  leo  wanapenda utendaji kazi  wake  hivyo kwa mwana Ludewa ambae hatataka  kuonyesha  ushirikiano basi ana lake  jambo  ila  kati ya  wapinzani ambao  wanatambua  mchango mkubwa wa maendeleo unaofanywa na mbunge  huyo ni pamoja na yeye .

Alisema kwa  kata  hiyo ya  Lupingu  toka utawala wa Filikunjombe umeanza mwaka 2010 kumekuwepo na mafanikio makubwa ya  kimaendeleo  ikiwa ni pamoja na wananchi hao  kuanza  kupata  usafiri wa uhakika  tofauti na awali  ambapo walikuwa  wakilazimika  kutembea  kwa  miguu na mizigo  kichwani kwa  zaidi ya kilometa 50  hadi  Ludewa mjini.

" Leo  wananchi wa Lupingu ambao tulikuwa  tukilia  kuwa  serikali  imetutelekeza na  wakati  mwingine  kuhisi kama tupo nchi ya Malawi  leo hii barabara  nzuri  imejengwa ,umeme   wa uhakika   unaletwa sasa Mungu atupatie  nini zaidi ya Filikunjombe ......nasema  wananchi wangu  tumehangaika  sana  kutafuta  mbunge  Ludewa na kila baada ya  miaka  mitano  tulikuwa  tukichagua  mbunge mwingine ila kwa  huyo wa sasa tunasema hatuhitaji mtu  mwingine  tunahitaji maendeleo kama  haya"




Kwa  upande  wake  mbunge  Filikunjombe mbali ya  kuwapongeza  wananchi hao wa kata ya  Lupingu kwa kuonyesha mfano wa  kujitolea   kuchimba mashimo  ya  kusimika  nguzo za umeme  pamoja na kufyeka  miti  inayopita  katika laini ya umeme  bado  alisema  wameonyesha  uhitaji mkubwa wa  umeme na  kuwa  wananchi  wa  pekee  nchini ambao  wamekubali  kufyekewa mazao na miti  yao  bila  kudai  fidia ili umeme  upite .

Kuhusu mradi huo wa umeme Filikunjombe  alisema kuwa kwa kasi  ambayo  wananchi  wanaenda nayo katika  kujitolea  nguvu  zao kuchimba mashimo na  kusogeza nguzo katika mashimo  hayo ni  wazi  mradi huo wa umeme  utakamilika kabla ya  Desemba mwaka  huu .
 
Aidha  alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010  ni  kijiji  kimoja pekee cha jimbo  hilo la Ludewa ambacho  kilikuwa na umeme  wa mafuta  ila  sasa  zaidi  ya vijiji 10  vina umeme na kuwa hadi sasa   jumla ya  vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu za  serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki Dayosisi ya  Njombe.


Alisema iwapo  wananchi  hao  wangekuwa kama  wale wa mijini ama mikoa mingine ambao wamekuwa  wakikwamisha  miradi kuanza kwa  wakati kutokana na kudai  fidia kwa  kila kitu basi  yawezekana umeme kufika Lupingu ungechukua muda  mrefu  zaidi hasa  kutokana na wingi wa  miti ,mashamba ya mihogo na mali  nyingine ambazo  zingepaswa  kufanyiwa tathimini  kabla ya  kuondolewa .

Kwani  alibainisha  kuwa haoni sababu ya yeye  kuendelea  kuishi mjini wakati  wapiga kura  wake  wana matatizo chunngu mzima   hivyo lazima akipata  muda wa mapumziko kukimbia  jimboni kuhamasisha maendeleo na kutekeleza ahadi  zake badala ya  kustarehe  mjini .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA