FIGO: NJOONI MUONE VITU VYANGU KESHO TAIFA, KAREMBEU ASEMA ATAMPA MAPANDE YA KUMWAGA AWABURUZE WATANZANIA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Luis Figo ameahidi burudani nzuri ya soka kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati magwiji wa Real Madrid ya Hispania watakapomenyana na magwiji wa Tanzania katika mchezo wa kirafiki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu katika hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam, mshindi huyo wa Ballon d’Or mwaka 2000, aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, amesema kwamba Watanzania watafurahia kazi yake uwanjani kesho.
Njooni muone kazi; Figo wa pili kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam

Figo aliyepiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia, amewaomba wapenzi wa soka Tanzania kujitokeza kwa wingi kesho kushuhudia burudani.
“Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, nimekwishatembea nchi kadhaa Afrika, nimefurahi kuja hapa, naipenda Afrika. Natarajia mchezo mzuri kesho, hata kwa wapinzani wetu pia, kitu muhimu ni kwamba FIFA imefurahia tukio hili,”alisema Figo.
Kwa upande wake, mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998, Christian Karembeu aliyeshinda Kombe la Dunia na Ufaransa mwaka 1998, amesema kwamba atampa pasi nyingi kesho Figo afanye vitu vyake.
Beki wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Fernando Sanz Duran ni miongoni mwa wanasoka watatu waliowika Real Madrid muongo uliopita waliofika jana usiku, ambaye pia alikuwepo kwenye mkutano wa leo.
“Nimefurahi kuja Tanzania, ni mara yangu ya kwanza, Watanzania watarajie burudani nzuri kutoka kwetu na wapinzani wetu,”alisema Sanz huku akimgusa begani, kocha Msaidizi wa Magwiji wa Tanzania, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa, anatarajiwa kuwasili katika kundi la mwisho la Magalactico hao jioni ya leo. 
Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ambao ndiyo wanawaleta magwiji hao nchini, amesema maandalizi yote yamekamilka na Watanzania wajitokeze kwa wingi Taifa kesho.
Magalactito wa Real wamefikia katika hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach wakati timu ya Tanzania imeweka kambi Kariakoo, Dar es Salaam kikiendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa.
Karembeu kulia na Figo kushoto wakifurahi na Mkurugenzi wa Makampuni ya TSN, Farough Baghozah
Kutoka kushoto Fernando Sanz, Karembeu, Figo na Farough 

Kikosi hicho kinaundwa na makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter, mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, 
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, 
Viungo Athumani China, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, 
Madaraka Suleiman na Akida Makunda. 
Benchi ka Ufundi, ni Kocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa.
Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.