HABARI MPASUKOOOOO!!!!!!!! JAJI LEWIS MAKAME AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia punde ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame (pichani) amefariki dunia leo katika Hospitali ya AMI , Masaki jijini Dar es Salaam alilokuwa amelazwa kwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

Jaji Makame ambaye kwa kipindi kirefu aliongoza NEC, alilazwa katika hospitali hiyo mwishoni mwa mwezi Julai. Rais Jakaya Kikwete alimtembelea kumjulia hali Julai 28, mwaka huu.

Kwa vipindi viwili, Jaji Makame akiwa Mwenyekiti wa NEC,  ndiye aliyetangaza matokeao ya uchaguzi Mkuu wa 2005 na 2010 ambapo Rais Kikwete aliibuka mshindi dhidi ya vyama pinzani.


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  leo, Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Lewis Makame aliyelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam Julai 28,2014.

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

Habari zaidi juu ya kifo chake tutawaletea baadaye.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*