JIONEEE SILAHA ALIZOKAMATWA NAZO WAZIRI WA ZAMANI WA ZANZIBAR


 Jumla ya Risasi 295 za Bastola ( Pistol) , marisau 112 ya bunduki ya Shortgun ( Gobore)  aliyokutwa nazo Mansour Yussuf Himid aliposachiwa nyumbani kwake
  Bastola na aina ya Bunduki ya Gobore wakioneshwa waandishi wa habari ( hawapo pichani)
 Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid akiwasili  mahakamni


 Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid akiiongea na baadhi ya watu mbalimbali
Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Mansour Yusuph Himid akiwa  Makao Makuu ya Polisi Zanzibar jana, baada ya kukamatwa nyumbani kwake, Chukwani kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume na sheria. Picha na Mwinyi Sadallah na Othman Mapara
------
  Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mansour Yusuph Himid amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matatu ya kupatikana na bunduki na risasi 407 kinyume na Sheria namba 2 ya 1991 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mansour alifikishwa mahakamani akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi  akisindikizwa na magari matatu huku askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakitanda eneo zima la Mahakama wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi.
Mwendesha mashtaka, Maulid Ame Mohamed alimsomea mashtaka matatu likiwamo la kupatikana na silaha kinyume na Kifungu 6(3) na 34(1)(2) cha Sheria ya Silaha na Risasi namba 2 ya mwaka 1991, Sura ya 223 ya Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alidai kwamba Agosti 2, mwaka huu saa saba mchana huko Chukwani, Unguja bila ya halali alipatikana na bastola aina ya baretta yenye namba F76172W kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Mwanasheria huyo akisaidiwa na Raya Mselem alisema kosa la pili ni kupatikana na risasi kinyume na Kifungu cha sita (3)(1)(2) cha Sheria ya Risasi za moto. Mshtakiwa alidaiwa kukutwa na risasi za moto 295 za bastola ambacho ni kinyume na sheria.
Kosa la tatu alilosomewa ni kupatikana na risasi nyingine 112 kinyume na Kifungu cha 32(2) cha Sheria ya Silaha na Risasi namba 2 ya mwaka 1992 ambayo inaruhusu kumiliki risasi aina hiyo mwisho 50 kwa matumizi ya silaha aina ya shortgun.
Waziri huyo wa zamani baada ya kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Khamis Ramadhan Abdallah Shaban aliyakana yote matatu.
Kabla ya kesi hiyo kuanza, Wakili Gasper Nyika anayemtetea alitakiwa kuonyesha vibali vinavyomruhusu kufanya kazi Zanzibar na kusababisha kesi kusimama kwa muda kabla ya hakimu kumruhusu kuendelea baada ya kuridhishwa na kibali chake.
Hata hivyo, Hakimu Khamis alisema shtaka la kwanza la kupatikana na silaha halina dhamana, tofauti na mashtaka ya pili na tatu ambayo yanaruhusu mshtakiwa kupata dhamana.
Wakili Nyika anayesaidiana na Omar Said Shaban alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Zanzibar, Kifungu cha 150 (4) namba 7 ya mwaka 2004,  Mahakama Kuu ina uwezo wa kupokea ombi la dhamana kwa kesi kama hizo kama mhusika atakuwa na sababu za kuishawishi mahakama kumpatia dhamana.
“Tunajiandaa kuwasilisha ombi letu la dhamana Mahakama Kuu na hilo litafanyika haraka. Bado mteja wetu ana haki ya kupata dhamana hiyo,” alisema Wakili Nyika.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Hakimu Khamis aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 na mshtakiwa kupelekwa rumande katika Gereza la Kiinua Miguu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.