MAULIDI KITENGE KUREJEA TENA HEWANI KESHO ATAKUWA NA PACHA WAKE KATANGA AMBAYE PIA AMEJIUNGA NA E FM



KITENGE WAKATI AKIKABIDHIWA MKATABA MPYA WA E FM.


Mtangazaji mpya wa E FM Radio, Maulidi Kitenge anatarajia kuanza kusikika tena hewani kesho Alhamisi.

Kitenge maarufu kama jezi namba 10 mgongoni anatarajia kuanza kusikika katika kipindi kipya cha redio hiyo ambacho kitakuwa kikirushwa saa 1 usiku, kila siku.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Kitenge ambaye ni mtangazaji maarufu wa michezo nchini alisema wako katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kipindi hicho saa moja kamili kesho Alhamisi.
 
“Maandalizi yanakwenda vizuri na Mungu akijaalia, Alhamisi tutaanza,” alisema Kitenge.

Kitenge na mtangazaji pacha wake, Katanga wamehamia E FM wakitokea Radio One.
 
Kitenge akifanya kazi Radio One kwa miaka 14 na siku nne zilizopita aliaga rasmi na kuanza makazi mapya na redio hiyo mpya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.