MUME NA MKE WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA




 Gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T.589 AZS likiwa limebeba magunia ya madawa ya kulevya aina ya bhangi mara baada ya kukamatwa eneo la Sanawari jijini Arusha na askari wa kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya mkoani hapa.Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
---

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewakamata  watu watano wakiwa na magunia saba ya madawa ya kulevya aina ya bhangi wakiwemo mke na mume. Awali askari wa Kitengo cha Kuzuia Madawa ya Kulevya Mkoani hapa wakiwa doria walipata taarifa toka kwa raia wema iliyoeleza kuwepo kwa watu wanaosafirisha madawa hayo.
Mara baada ya kupata taarifa hiyo askari hao waliweka mtego maeneo ya Sanawari ambapo muda wa saa 3:30 usiku walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Hussein Rashid (35) mkazi wa Sakina, dereva pamoja na mwenzake Sebastian Wilbert (37) Fundi magari, mkazi wa Ilboru wakiwa wanasafirisha magunia matano ya madawa ya kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 171 kuelekea nchi jirani ya Kenya kwa kutumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T. 589 AZS.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, mara baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa walikiri kosa hilo na kumtaja mwanamke aitwaye Flora John (38) Mkazi wa Ekenywa- Ngaramtoni kuwa ndio aliyewauzia.
Kamanda Sabas aliendelea kwa kusema kwamba, askari hao walianza kumfutilia mwanamke huyo ambapo jana Jumanne tarehe 05.08.2014 walikwenda nyumbani  kwake na kumkuta mtuhumiwa ambaye ni muuzaji akiwa na mume wake aitwaye John Meleji (45) Mkazi wa Ekenywa na mara baada ya kufanya upekuzi walikuta gunia moja la madawa ya kulevya aina bhangi ndani ya nyumba hiyo.
Mbali na kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni mke na mume pia askari hao walimkamata jirani yao aitwaye Loseriani Metelami (21) Mkulima mkazi wa Ekenywa baada ya yeye pia kukutwa na gunia moja la madawa ya kulevya aina ya bhangi hivyo kufanya jumla ya magunia yaliyokamatwa kuwa saba.
Watuhumiwa hao watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni mara baada ya upelelezi kukamilika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI