MWANAMKE ZITAMBUE NJIA 18 ZA KUITEKA AKILI YA MWANAUME HASA KATIKA TENDO LA NDOA KUDUMISHA UPENDO.

FUATILIA SOMO HII KWA UMAKINI.
Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika.

1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k

2.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" 
 
"Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.

3.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.

4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.

5.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.

6.
Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula chako.
 
Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.

7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.

8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.

9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.

10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe.

11.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.

12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi 
yako.

13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.

14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.

15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.

16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.

17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.

18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI