PAPA FRANCIS AJITABIRIA KIFO


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu.

 Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba
alisema.Papa Francis (77), pia alizungumzia uwezekano wa kustaafu endapo atahisi kwamba afya yake hairuhusu kuendelea na kazi. 
 
Utamaduni wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa Benedict XVI aliyeng’atuka kutokana na matatizo ya kiafya.Pamoja na kwamba Papa Francis hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu ni lini pengine anaweza kufariki dunia, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka Vatican vinasema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia duniani. 
 
Wachambuzi wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.Wakati hayo yakiendelea taarifa za ndani zinabainisha kwamba kiongozi huyo aliwahi kutolewa pafu moja baada ya kuathirika wakati akiwa kijana nchini Argentina

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.