SAKATA LA UHAMIAJI KUPEANA AJIRA MOTO WAZIDI KUWAKA,KAMATI YA KUCHUNGUZA YAITWA

Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za upendeleo katika utoaji nafasi za ajira 200 kwa watu waliyoomba nafasi hizo kupitia idara ya uhamiaji imebaini kuwa nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo bila ya kufuatwa taratibu, kanuni na sheria ya utoaji wa ajira hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil amesema  kamati hiyo imeweza kubaini kuwa mambo mengi yalifanywa  kiujuma jumla sana na hivyo kutoa mwanya wa watu kupindisha mambo.



Kamati hiyo iliundwa Agosti Mosi mwaka huu, chini ya watu watano ikiongozwa na yeye mwenyewe katibu mkuu wa wizara ya  hiyo.
Iadha katika mkutano huo jeshi la polisi kupitia mkurugenzi wa makosa ya jinai kamanda Isaya Mngulu amesema jeshi hilo litafanya operesheni ya kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wakiwemo waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya kuwaua ama kuwajeruhi walemavu wa ngozi kwa imani zao za kishirikina.

CHANZO: ITV TANZANI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.