Serikali yasema hakuna Ebola Tanzani

a
Tanzania imesema haina mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.Kauli hiyo inakuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid ameiambia BBC, wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania, lakini vipimo vimeonesha hawana maambukizo hayo.

Amesema tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.
Mafunzo yametolewa pia kwa wataalamu watakao hudumia wagonjwa iwapo watatokea.
Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa, vimewekwa pia.
Wizara ya Afya ya Tanzania inaongeza uwezo wa kufanya uchunguzi, katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.
CHANZO:BBC

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*