SIMBA WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL DAR

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
SIMBA SC ambayo iko katika shughuli mbalimbali za kuadhimisha Simba Week imefanya ziara  ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza bia cha TBL kinachozalisha bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayoidhamini timu hiyo.
Akiongea katika ziara hiyo  Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa wao kama timu ya Simba wameamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao kutembelea wadhamini kila mwaka ili kuimarisha uhusiano na wadhamini na kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio wadhamini wakuu wa timu yao.
Wachezaji wa Simba SC wakiwa TBL jana
Meneja wa Kilimanjaro, George Kavishe akifurahia jambo na kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda kulia

Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika mambo mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo hivyo wamefurahishwa sana na jinsi walivyopokelewa vizuri kiwandani hapo na aliwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
Akiongea kwa niaba ya kampuni hiyo Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo hiki cha timu hii ya Simba kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao na kuona kazi ambazo zinafanywa na kampuni hii.
Alisema kuwa TBL inathamini mchango wa timu za Simba na Yanga kwa soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikizidhamini timu hizi kwa muda mrefu huku akibainisha kuwa wataendelea kudhamini timu hizi hadi mwisho.
Alibainisha kuwa timu hizi mbili zimekuwa zikifanya mambo makubwa kwani zimekuwa zikiwapatia vijana mbalimbali ajira kwa kupitia timu zao.
Aliwasihi wananchi kwa ujumla kuendelea kuisapoti timu hizi kwani ndio timu mbazo zina wachezaji wengi zaidi wanaochezea timu ya taifa.
Kavishe alisema kuwa kupitia kudhamini timu hizi pia wamekuwa wakijitangaza sehemu mbalimbali kwani iwapo timu ikienda kucheza nje ya nchi wanaenda kukitangaza kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager hivyo wanafanya  kampuni hii pamoja na bia ya Kilimanjaro kuwa juu zaidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU