WASANII WATAKAOTUMBUIZA TAMASHA LA FIESTA 2014 JIONI YA JIJINI TANGA WAMJULIA HALI MZEE NJENJE NYUMBANI KWAKE SAHARE

 Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa. 
Mzee Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na kuitangaza nchi kwa ujumla.
 Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.
 Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya,Alli Kiba akizungumza jambo na Mzee Njenje. 
Mzee Njenje akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakaotumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 linalofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Wasanii hao walikwenda kumsabahi mkongwe huyu wa Muziki hapa nchini,Nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga ambako ndiko anaendelea kupata matibabu yake ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa,Mzee Njenje amesema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika kadiri ya siku zinavyozi kwenda.  
 Baadhi ya Wasanii mbalimbali ambao Watatumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani ,wakiwasili nyumbani kwa Mzee Njenje,Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga kumjulia hali.Picha zote na Michuzi Jr-FIESTA TANGA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU