Skip to main content

WATU WAWILI WAFA ,52 WAJERUHIWA AJALI YA BASI SINGIDA

 

DSC00462
Mwili wa abiria wa kike anayedaiwa kuwa na umri katika ya miaka 20-23 aliyefariki dunia kwenye ajali ya basi la KISBO iliyotokea katika kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.

DSC00457
Askari wa usalama barabarani wilaya ya Ikungi, akikagua basi la kampuni ya KISBO, T.534 CHX baada ya kupinduka katika eneo la kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 52.
Na Nathaniel Limu, Singida
ABIRIA wawili wamefariki dunia na wengine 52 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka.
Basi lililohusika na ajali hiyo ni T.534 CHX aina ya Scania mali ya kampuni ya KISBO. Ajali hiyo inayodaiwa kuchangiwa na mwendo kasi ,imetokea Agosti 21 mwaka huu saa 9.45 alasiri huko katika kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna,wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela  alisema watu hao waliopoteza maisha yao papo hapo,ni kijana wa kiume ambaye alikuwa konda wa basi hilo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 23 na abiria wa kike anayekadiriwa kuwa na umri huo huo wa kati ya miaka 20-23.Wote wawili hadi sasa majina yao bado hayajulikana.
Alisema basi hilo lililokuwa linatokea Dar-Es-Salaam likielekea Kahama mkoa wa Singida, lilipofika eneo la tukio lilipasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka mara moja na kuserereka hatua zaidi ya mia moja.
DSC00459
Basi la kampuni ya KISBO T.534 CHX linavyoonekana baada ya kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka katika kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.
Alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Edward Paulo Temu (45) mkazi wa jijini Dar-es-salaam ambaye inadaiwa siku hiyo ndiyo alikuwa amekabidhiwa rasmi kuendesha basi hilo.
Kamwela alisema katika ajali hiyo, abiria 52 kati yao 20 wamelazwa katika hospital ya Misheni ya Puma na wengine 32 wamelazwa katika hospitali ya mkona mjini hapa.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha wazi kuwa basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi. Naomba nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wananchi kufika katika hospital ya mkoa ,ili kuwatambua marehemu kwa ajili ya kufanya taratibu za mazishi.
Kwa upande mwengine natoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara,kufuata sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani kama njia moja wapo ya kupunguza ajali zinazochangia rai kupoteza maisha na mali zao”,alisema Kamanda Kamwela.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Deogratius Baluba alikiri kupokea miili ya watu wawili waliofariki kwenye ajali ya basi la KISBO na majeruhi 32 ambao wengi hali zao zinaendelea vizuri.
Katika hatua nyingine,Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone aliyefika kwenye eneo la tukio akifuatana na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Alhaji Manju Msambya walionyesha masikitiko yao kutokana na ajali hiyo na kutosita kukemea tabia ya baadhi ya madereva wanaokwenda mwendo kasi unaosababisha ajali na vifo vya abiria.
DSC00466
Askari wa usalama barabarani wakuchukua maelezo kutoka kwa mmoja wa majeruhi (amelazwa katika hospitali ya mkoa) wa basi la KISBO T.534 CHX aina ya Scania lililopinduka baada ya kupasuka tairi katika eneo la kijiji cha Kambi ya mkaa wilaya ya Ikungi.(Picha zote na Nathaniel Limu).
DSC00468

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.