WAZIRI KAMANI ANG'ARA KIMATAIFA, APEWA TUZO


Na Mwandishi Wtu
WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani (Pichani), amepewa Tuzo ya Utawala Bora katika kipengele cha Watendakazi Bora Serikali barani Afrika kutokana na wizara yake kuonyesha utendaji kazi wa hali ya juu.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Kampuni ya CEO Titans Building Nations ya Afrika Kusini, ambayo imejikita katika kutambua watu na viongozi wanaofanya kazi kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Hilton jijini Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam, juzi jioni mbali na Dk. Kamani, mwingine aliyepata tuzo hiyo ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu, aliyenyakua tuzo ya Uongozi Thabiti katika Vyombo vya Habari vya Tanzania.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dk. Kamani alisema hiyo ni ishara ya kuwa serikali na watendaji wa wizara yake wanawajibika kikamilifu.

Alisema wizara yake ina jukumu la kusimamia maendeleo ya mifugo sekta ambayo, imekuwa mkombozi mkubwa wa Watanzania wengi na kuwa, amefarijika kuona utendaji wa wizara yake ukitambulika kimataifa.

“Wakati naalikwa kuhudhuria hafla hii nilijua ni masuala ya utendaji ila sikufahamu kama kuna tukio hili la jitihada za wizara yangu kutambuliwa. “Nimefarijika kuona kazi yetu inatambulika hivyo, tutaendelea kuongeza bidii zaidi ili kutimiza azma yetu ya kuwainua wafugaji na wakulima kwa ujumla kiuchumi,” alisema Dk. Kamani.

Washiriki 100 kutoka taasisi mbalimbali barani Afrika walichaguliwa, ambapo wawakilishi 28 waliingia fainali kuwania tuzo katika nyanja tofauti.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI