KIKWETE AMVALISHA CHILIGATI ‘KIATU’ CHA MAKINDA…!

      

Capt. John Chiligati ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Kamati mpya ya Uongozi ya Mkurabita
Capt. John Chiligati ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Kamati mpya ya Uongozi wa Mkurabita
“NIMSHUKURU Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kwa kuniona na kuniamini na hivyo, kuniteua ili niweze nami kuvaa kiatu anachokiacha Mheshimiwa makinda”. Anasema, Kapteni Mstaafu wa John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika hafla ya uzinduzi wa Kamati mpya ya Uongozi wa Mpango wa Kuratibu na Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) na kuwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo waliomaliza muda wao.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Dar es Salaam Serena jijini Dar es Salaam, Chiligati ambaye ameteuliwa na Rais Kikwete hivi karibuni kuwa Mwenyekiti wa Kamati mpya ya Uongozi ya Mkurabita akichukua nafasi iliyotumikiwa kwa takriban miaka 10 na Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, akasisitiza, “Kwa mtazamo tu wa haraka, kiatu hiki ni kikubwa kweli kweli, lakini naamini kwa ushirikiano kutoka kwa wajumbe wenzangu, watendaji wa Mkurabita, Waziri na Ikulu yote pamoja na wadau wote na wapenda maendeleo, tutaweza kutekeleza kazi hii kwa ushindi mkubwa.”
Anaongeza, “Hii ni kwa kuwa kweli nimeona nia thabiti ya Serikali ya kutaka kuinua uchumi wa nchi yetu kupitia rasilimali ardhi na biashara halali zinazoendeshwa na Watanzania…” Mwenyekiti huyo (Chiligati) alisema katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kamati mpya kuwa, endapo Mkurabita utaeleweka zaidi kwa umma na malengo yake kutekelezwa ipasavyo, uchumi wa nchi utaimarika. Akasema, “Naomba Mungu atusaidie mimi na wenzangu ili nia hii ya kusisimua uchumi wa nchi yetu kupitia urasimishaji iweze kuwa ya kweli.”
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita aliyemaliza muda wake, Anna Makinda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita aliyemaliza muda wake, Anna Makinda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita inayomaliza muda wake, Anne Makinda akasema lengo la Serikali kuanzisha Mkurabita ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutumia rasilimali na biashara zao ambazo ni rasmi. Akasema, “Mkurabita imepewa wajibu wa kuhakikisjha rasilimali na biashara zinazoendeshwa nje ya mfumo unaotambulika kisheria zinakuwa rasmi na hivyo, kutambulika kisheria.”
“Matokeo ya tathmini ya sekta isiyo rasmi iliyofanywa na mtaalamu kati ya mwaka 2004 na 2005 yalionesha kuwa, asilimia 89 ya ardhi na asilimia 98 ya biashara hazikidhi matakwa ya kisheria. Thamani ya rasilimali hizi ni jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 29. 3 alizozitaja kuwa ni mtaji mfu.”
Kwa mantiki hiyo, Makinda alisema kazi ya kurasimisha rasilimali hizo inategemewa kufufua mtaji huo mfu na kuufanya kuwa mtaji hai utakaochangia kikamilifu ukuaji wa uchumi wa taifa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*