MBUNGE GODFREY MGIMWA ASEMA AMETUMIA ZAIDI YA TSH MILIONI 68 KWA MIENZI MITATU YA UBUNGE WAKE KUTEKELEZA AHADI 90 ZA MBUNGE WA KALENGA ALIYEFARIKI DUNIA DR WILIAM MGIMWA


Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  (kulia) akikabidhi ahadi ya bati 100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr  Wiliam Mgimwa kwa  viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa  shule ya msingi Lukwambe hadi  sasa ni asilimia 90 ya ahadi binafsi za mbunge aliyefariki  zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge Mgimwa
mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea  ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Diwani wa kata ya Ulanda kulia  akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Mgimwa  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Katibu  wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa  kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa 
Mwananchi  wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga  Bw Godfrey Mgimwa
Mbunge Mgimwa akidua sanjari na  wananchi wa kijiji cha Mangalali 
Mmoja kati ya  wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa  utendaji kazi mzuri 
Katibu wa Mgimwa akiwaonya  wana CCM wanaojipitisha  jimboni kwa  sasa 
Baadhi ya Wananchi wa  kijiji  cha Mangalali  wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa



Mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kulia akikabidhi mchango wake wa Tsh 250,000 kwa ajili ya kusaidia kazi ndogo ndogo  za ujenzi wa zanahati ya kijiji cha Mangalali 
 .......................................................................................................
Na Matukiodaima.co.tz
MBUNGE   wa  jimbo  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  ajipongeza kutumia kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya  kufanikisha  utekelezaji wa ahadi  zilizotolewa na mbunge  aliyefariki Dr  Wiliam Mgimwa  kwa  asilimia 90 kwa  muda  wa  miezi mitatu pekee .

Akizungumza na  wananchi  wa  kijiji  cha Mangalali   baada ya  kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa  alisema  kuwa alianza  kutekeleza  ahadi hizo hata kabla ya  kuapishwa   bungeni na  hadi sasa  bado asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge  aliyefariki  dunia mwanzoni mwa mwaka  huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi.

" Ni jambo la kumshukuru  mwenyezi Mungu  kwani ahadi  zilizokuwa  zimetolewa na  mbunge  aliyefariki  dunia marehemu Dr  wiliam Mgimwa  zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua  kuwa  mbunge ahadi  hizo  zilikuwa  bado kutekelezwa na ndio  sababu ya mimi   katika kampeni kutoahidi  ahadi mpya  zaidi ya  kuzipokea  zile  zilizoachwa na baba ambazo  kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi  hizo nimetekeleza kwa asilimia 90  bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani  nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea  uzima" alisema  mbunge Mgimwa.

Alisema  kuwa hakuweza  kuahidi ahadi mpya  wakati wa kampeni  hizo za uchaguzi mdogo  jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo  zilikuwa zimetolewa na mbunge  aliyepita na zilikuwa bado  kutekelezwa na muda  wa   utekelezaji  ulikuwa bado  hivyo aliamua  kuzichukua  zote kama  zilivyo na kuanza  kuzifanyia kazi moja baada  ya nyingine .

Mbunge Mgimwa alisema  kuwa ahadi  hizo  zinazotekelezwa  ni  zile ahadi  binafsi ambazo mbunge  aliyepita alikuwa amezitoa ila  zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya  CCM ambazo pia  zimeendelea  kutekelezwa  kwa  nguvu  kubwa .

Hata  hivyo  alisema kuwa ahadi ambazo  zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja  na elimu ,afya na  uchangiaji wa  vikundi  vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa  vikundi  hivyo pia katika  sekta ya  michezo na huduma  nyingine  za kijamii kama  upelekaji wa umeme katika maeneo ya kata ya Mgama  na Magulilwa zoezi hilo  linaendelea ambayo   ahadi  hiyo ya umeme  ipo katika ilani ya CCM pamoja na zile za  huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi kata ya Maboga  na kata ya Lumuli wa maji  unatekelezwa .

Pia  alisema  kuwa bado  anautamani  ubunge wa  jimbo  hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020   hivyo kamwe hatawaangusha  wana Kalenga kwa  kipindi  hiki  cha miaka miwili alichopewa  hadi 2010.

" Ndugu  zangu hii nafasi ya  ubunge  mimi  nimeipata mwishoni ila sikutaka  kuwaangusha  nilitaka kuwaonyesha  utendaji  wangu na kamwe  sitakuwa mbali na ninyi  wananchi  wangu  nitakuwa  bega kwa  bega  kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni  jimbo la mfano katika maendeleo  kule  bungeni kutokana na umri  wangu  wabunge  wananiita bwana mdogo ila  kiutendaji kweli  ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni  mimi ni mmoja kati ya  wabunge  tuliochanguliwa  kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya  serikali " alisema mbunge Mgimwa .

Awali katibu  wa mbunge huyo  Martine Simangwa  aliwaonya  wana CCM ambao  wameendelea  kujipitisha katika  jimbo  hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki  wananchi wa  jimbo la Kalenga ambao kwa  sasa wameshikamana na  wapo tayari kuona  maendeleo na sio kampeni za  uchaguzi wa mwaka 2010.

"  wapo  baadhi ya  wana CCM bila haya  wameendelea  kujipitisha kwa wananchi na  kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa  wananchi  nawaombeni  sana msidanganyike na  watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa  pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini  kuungana katika misingi ya kimaendeleo"

Kwa upande  wao  wananchi hao  walieleza  kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge  wao Mgimwa na  kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa  wamejipanga  kumchukulia  fomu mwakani  ili kuwaongoza vipindi  vingine viwili zaidi baada ya  kuona utendaji  wake mzuri.

MWISHO 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI