Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Rose Mang’enya wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba na Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Eleuteri mangi (kulia).
Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya na kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba.Picha na MAELEZO
……………………………………………………
BeatriceLyimo- MAELEZO
Taasisi isiyo ya kiserikali ya MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi katika jamii ya Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa madhumuni ya kujenga uchumi.

Meneja Masumba amesisitiza kuwa MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja kwa mwezi juu wafanyakazi kufanya maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu 600 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha waandishi wa habari juu ya yaliyomo kwenye kitabu hicho kwa kuendesha warsha fupi iliyowafungua macho waandishi hao kuhusu namna ya kutunza fedha kuandaa maisha ya baadaye.
Akinukuu kauli ya mtaalamu wa uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa “Watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa hawatofautiani sana kiuwezo bali wanatofautiana katika dhamira ya kufika kilele au upeo wa uwezo wao”.
Mang’enya aliongeza kuwa jukumu la kujenga maisha binafsi   lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.
Aidha, MAYEPS hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Umama na binafsi namna ya kupanga matumizi.
Pia hutoa mafunzo ambayo yatawezesha wafanyakazi kutambua kuwa fedha za mafao au pensheni hupungua thamani mwaka hadi mwaka hivyo uwekezaji wa fedha hizo ni muhimu ufanywe kwa uangalifu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.