SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA TECH YASAIDIWA KUMALIZA KERO YA MASHINE YA PRINTA NA MBUNGE MGIMWA


Mkuu  wa  shule ya  sekondari ya  Ifunda Tech Bw  Maddy  Kissuo akipokea  msaada wa  fedha  kiasi cha Tsh milioni 2  kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa kwa ajili ya kuiwezesha  shule hiyo  kununua mashine ya Printa
Mbunge wa Kalenga  akiwa ameonyesha  ishara ya dule ngumba  kama  ishara ya kuwapa moyo  wanafunzi hao kusoma  zaidi japo  ishara  hiyo pia inatumiwa na CCM inasemana kama neno "kidumu"

Mkuu wa  shule ya  sekondari ya Ifunda Tech akishukuru kwa msaada  huo wa mbunge Mgimwa
Mbunge wa  jimbo la kalenga Dofrey Mgimwa akisaini kitabu cha wageni katika  shule ya sekondari Ifunda Tech baada ya kufika  kutimiza ahadi yake ya  fedha kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya Printa 
Mbunge Mgimwa kushoto akizungumza na wanafunzi wa sekondari ya Ifunda kabla ya kumkabidhi mkuu wa shule hiyo Maddy Kissuo (kushoto kwake )fedha  kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya Printa shuleni hapo 
Katibu  wa mbunge wa jimbo la kalenga Bw Martine  Simangwa kushoto akijitambulisha kwa  wanafunzi wa sekondari ya Ifunda katikati ni mbunge Mgimwa na  kushoto ni diwani wa kata ya  Ifunda Elia Mgwila
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ifunda  wakimsikiliza kwa makini mbunge Mgimwa (hayupo pichani)
Mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Ifunda Tech
Picha na habari na Francis Godwin Blog
UONGOZI  wa  shule ya  sekondari ya  Ifunda Teck sec School  umempongeza mbunge  wa  jimbo la kalenga  Bw Godfrey  Mgimwa  kwa  kutekeleza ahadi yake ya fedha taslim kiasi cha Tsh milioni 2 kwa  ajili ya kusaidia ununuzi wa mashine ya Printa katika  shule  .

Mkuu  wa  shule hiyo Maddy Kissuo alitoa  pongezi hiyo jana  mbele ya  mbunge  Mgimwa baada ya  kupokea msaada  huo wa Tsh milioni 2 zilizoombwa na uongozi wa  shule  hiyo mwanzoni mwa mwaka huu wakati wa mahafali ya kidato  cha  sita  .

Alisema  kuwa  mbunge  huyo ameonyesha mfano  wa kuigwa na viongozi wengine katika  kutekeleza ahadi zao kwa  wakati na kuwa  bila msaada  huo  uwezekano wa  shule  hiyo kupata fedha za kununua mashine  hiyo ulikuwa mgumu  zaidi hasa ukizingatia na hali ya uchumi wa  sasa  shuleni  hapo.

"Jitihada  hizi  za mbunge  kutusaidia  mashine hii  ya printa  ni kubwa  sana na kuifanya  shule  hiyo kwa  sasa  kuwa na uhakika wa  kuchapa mitihani  mbali mbali  na  kuiprinti  hapo hapo  shuleni  tofauti na awali tulivyokuwa  tukisafiri hadi mjini Iringa umbali wa kilomita zaidi ya 50 kwenda  kuprinti mitihani ....kweli tunakuombea zaidi na zaidi  ili uzidi  kuendelea  kuwatumikia wananchi wa kalenga "alisema

Huku  Mbunge  Mgimwa akidai  kuwa amelazimika kuomba  ruhusa mara  moja ya siku moja bungeni Dodoma   ili  kurudi  jimboni kutimiza ahadi yake  hiyo ambayo alikuwa ameahidi  kuitimiza ndani ya mwezi  huu wa Septemba.

Akizungumza na   wanafunzi  wa  shule ya  sekondari  Ifunda baada ya kukabidhi msaada  huo alisema  kuwa amelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya fedha za kununua mashine ya  kuprinti mitihani shu;leni hapo kama ambavyo  uongozi wa  shule  hiyo  ulivyomuomba  wakati wa mahafali ya kidato cha sita  shuleni hapo mwaka  huu.

Hivyo  alisema isingependeza kama   ahadi hiyo  ingeendelea kuchelewa kutolewa shuleni hapo hasa  ukizingatia  kuwa mashine   hiyo  ina mchango  mkubwa katika  maendeleo  ya taalum shuleni hapo.

Kwani  alisema  kuwa  shule  kama  hiyo  kukosa mashine  kama  hiyo ni aibu  kubwa na ni  mwanzo wa taalum shuleni hapo  kushuka   kwa  walimu  kupoteza  muda  kwenda mjini zaidi ya kilometa 50 kutoka  shuleni hapo kwenda  kupata   huduma  hiyo ya mashine ya kuprinti mitihani ya  wanafunzi .

  Alisema  kuwa  wakati  yeye kama mbunge anatimiza ahadi  yake katika  shule  hiyo kwa ajili ya  wanafunzi hao ni  vema kwa upande  wao  wanafunzi  kuendelea  kudumisha nidham na kujituma zaidi katika masomo  ili ikiwezekano shule  hiyo kujakutoa kiongozi  bora  wa nchi mbeleni.

" Nawaombeni sana  wanafunzi someni  kwa  bidii na epukeni sana  vurugu  zisizo na maana katika maisha  yenu .....mimi kama  mbunge  wajibu  wangu  kwenu ni  kuwawakilisha bungeni ila  pia  kuwa karibu na  shule  yenu  hii pale mnapokwama  mimi nipo tayari  kuwasaidia"

Pia  alisema mategemeo  yake  kuona  shule  zake katika  jimbo la kalenga  zinaendelea  kufanya  vema katika  mitihani mbali mbali ya  kitaifa  ili ikiwezekano jimbo la kalenga  kuwa  kitovu cha  elimu kwa mkoa wa Iringa .



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.