TAARIFA MUHIMU KWA VYOMBO VYA HABARI

UONGOZI wa Tone Multimedia Company Ltd ambao ndiyo wamiliki wa Mtandao wa Blogs za Mikoa Tanzania www.blogszamikoa.blogspot.com ukiwemo wa Mbeya yetu www.mbeyayetu.blogspot.com unapenda kuwataarifu wadau wake wote hususani Wahariri wa Magazeti na redio mbali mbali za Mkoani Mbeya na  nchini kuwa wanaposoma na kuchukua habari kwenye mitandao yetu wajaribu kuandika au kutaja chanzo chake.
 
Tumelazimika kutoa taarifa hii baada ya kuwepo kwa Vyombo vya habari vikubwa kuwa na tabia ya kukopi na kutumia habari za kutoka Mbeya yetu na Blogs zengine za Mikoa bila kutaja wapi walikoipata hiyo habari.
 
Kiukweli hali hiyo inatusononosha kutoka na mazingira ambayo tunakuwa tumeyapata pindi tunapofuatilia matukio mbali mbali ikiwemo kuhatarisha maisha na usalama pamoja na gharama tuzitumiazo katika kufuatilia habari husika.
 
Aidha Mtandao wa Mbeya yetu haukatazi kwa Media yoyote iwe nje au ndani ya nchi kutumia habari zetu na ndiyo maana hazijafungwa hivyo ombi letu kwenu wadau ni kuandika chanzo chako cha habari ni wapi hiyo inachangia sisi kuona wewe mdau wetu umetambua mchango wa Mbeya yetu.
 
Hata hivyo Uongozi pia unatoa rai kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla kuthamini mchango wa vyombo vidogo na vya chini vinavyofanya kazi za kijamii kama ilivyo kwa Mtandao wa Mbeya yetu.
 
Hivyo basi kwa mantiki hiyo, Uongozi wa Mbeya yetu unapenda kuwataarifu hautasita kuwachukulia hatua za kisheria wale  wote watakaotumia taarifa za Mbeya yetu na Blog za Mikoa zinazomilikiwa na Tone Multimedia bila kutaja chanzo chake.
 
Tunategemea ushirikiano kutoka kwenu katika kuikomboa jamii ya Kitanzania na mahitaji walionayo na michango ya vyombo vya habari kwa jamii husika.
 
Imetolewa na Uongozi wa Tone Multimedia Company Limited,

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*