Tangu kuanzishwa shule ya Southern Highlands hakuna mwanafunzi aliwahi kufeli




Mkurugenzi mtendaji wa shule ya msingi Southern Highlands Bi Mary A. Mungai,akifungua mahafali hayo
Wahitimu wa shule ya shule ya msingi Southern Highlands, wakisoma risala
Wahitimu wa darasa la saba shule ya shule ya msingi Southern Highlands
Mkuu wa shule ya shule ya msingi Southern Highlands, Jason Nyabuto akizungumza wakati wa mahafali
 
Na Mathias Canal, Kwanza jamii-Mufindi
Hayo yamebainika wakati wa mahafali ya 14 ya shule ya msingi Southern Highlands iliyopo katika Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo Mkuu wa shule hiyo Jason Nyabuto amempongeza mkurugenzi wa shule hiyo kwa juhudi kubwa anayoifanya ili kuhakikisha wanafunzi wote wanasonga mbele kitaaluma ikiwa ni pamoja na kusoma mchepuo wa Sayansi kwa kadri ya namna wanavyofundishwa shuleni hapo.
Nyabuto alisema kuwa juhudi za wazazi/walezi na walimu ndio nguzo na uimara wa kukua kwa ufanisi wa taaluma shuleni hapo.
Alisema wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2014 walianza masomo yao Januari, mwaka 2008 huku idadi yao ikiwa ni wanafunzi 48 na kuhitimu idadi hiyo hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shule ya msingi Southern Highlands Bi Mary A. Mungai, aliwapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu elimu ya msingi shuleni hapo na kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto hao kuwa, elimu waliyoipata shuleni hapo ni ukombozi mkubwa kwa watoto hao na ukombozi wa Taifa kwa ujumla katika ufanisi wa elimu.
Amesema kuwa mapema mwaka 2015 wataanzisha shule ya Sekondari kuanzia kidato cha Kwanza hadi cha Sita lengo ikiwa ni kuendeleza ufanisi mkubwa wa elimu katika Wilaya ya Mufindi sambamba na Mkoa wa Iringa.
Mungai amesema kuwa kila mwaka mwezi wa sita wanafunzi wote hupata nafasi ya kusafiri kimasamo (Studying Tour), lengo ikiwa ni kukamilisha nguzo kuu tatu za elimu ambazo ni Kunusa, kuona pamoja na kugusa.
Shule ya msingi Southern Highlands haijawahi kufelisha wanafunzi tangu ilipoanzishwa mwaka 1994 na kupata usajili mwaka 1997.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1994 ikiwa inatoa elimu ya awali ( Chekechea) kabla ya kuanza kutoa elimu ya msingi.
Hata hivyo shule hiyo wakati inaanzishwa ilikuwa ikijulikana kama Lusungu Day Care Center ,ambapo baada ya kuanzishwa imekuwa na usajili kwa namba IR03/7/001 huku ikiwa ni shule ya pili kufunguliwa baada ya Brook Bond.
Mungai alisema tayari wamefungua shule ya awali katika kijiji cha Ihongole ili kupunguza usumbufu wa umbali waliokuwa wanaupata watoto mbalimbali kutoka maeneo hayo.
Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo Afisa elimu Mkoa wa Iringa Naseeb Mengela, amewapongeza wanafunzi hao kwa kumaliza elimu ya msingi na kuwasihi wazazi kutobweteka na elimu waliyoipata badala yake wawatafutie masomo ya ziada (Tuition) wakati wakiwa wanasubiri matokeo yao.
Mengela alisema kuwa Serikali haina budi kushirikiana kwa kina na shule za binafsi kwa kuwa zina mchango nkubwa katika kukuza elimu nchini na kuitambulisha elimu ya Tanzania kitaifa na kimataifa
Sambamba na hayo mgeni rasmi amewakabidhi wanafunzi wote vyeti vya kuhitimu ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi zawadi wanafunzi wote waliofanya vizuri ambao ni Osiah Ngombe aliyefanya vizuri kwa mwaka mzima, Gladness Ndemo kwa kuongoza somo la Hesabu, Mohamed Daud kwa kuongoza somo la Sayansi na Kiingereza, sawia na Mariam Iddy aliyefanya vizuri katika somo la Kiswahili.
Mgeni rasmi pia ametoa vyeti vya somo la Ngamizi (Computer), kwa wahitimu wote 48 kwani hakuna aliyefanya vibaya katika somo hilo.
Pia wanafunzi waliofanya vizuri kwa nafasi ya ya kwanza, pili na mwanafunzi ambaye alikuwa hafanyi vizuri lakini hadi anamaliza ameweza kufanya vizuri kwa kuwa nafasi ya tatu katika masomo ya Sayansi na Hesabu wamepata zawadi ya cheti na fedha kutoka kwa Christine Hellela, ambaye ameanzisha mfuko wa kusaidia wanafunzi wanaofanya vizuri kwa muktadha wa kumbukumbu ya mama yao Lucy Chawe.
Kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri na kuwa nafasi ya kwanza katika masomo hayo amepokea fedha taslimu shilingi 80000, nafasi ya pili 60000 na nafasi ya tatu 40000.
Hellela ameongeza kuwa kwa sasa wameanza kutoa zawadi kwa shule moja ya Southern Highlands, lakini mfuko ukiongezeka kadri ya matarajio yao watatoa zawadi kwa shule zingine pia.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA