Kufuatia
hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola kuweza kupenya nchini Tanzania na
kuleta madhara kwa wananchi wake, serikali ya Tanzania kupitia wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imeanza kutoa elimu ya dalili za ugonjwa huo na
namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi yake.
Tayari
mabango yenye ujumbe huo yamebadikwa katika vituo vya daladala jiji Dar
es Salaam na wananchi wamekuwa wakipita na kuyasoma mabango hayo na
kupata elimu.
Father
Kidevu Blog imeshuhudia mabangpo hayo katika kituo cha Msalaba Mwekundu
(Red Cross) kilichopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Comments