UJERUMAINI WAICHAPA SCOTLAND 2-1 SAFARI YA EURO



Special moment: Scotland winger Ikechi Anya places the ball past Germany goalkeeper Manuel Neuer to equalise for the Scots against the current world champions

Kitu kambani: Winga wa Scotland, Ikechi Anya akipiga mpira uliompita kipa wa Ujerumani  Manuel Neuer na kuisawazisha bao.
MABAO mawili ya Thomas Muller yalitosha kuwapa ushindi Ujerumani dhidi ya Scotland katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016 (Euro 2016).
Muller alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18 ya mchezo, lakini Ikechi Anya akaisawazishia Scotland katika dakika ya 66.
Baada ya matokeo kuwa 1-1, Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia chini ya kocha Joachim Low walifanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Wascotish na katika dakika ya 70, Muller aliandika bao la pili na la ushindi.
Muller alifunga goli lake la 24 na 25 katika mechi 58 alizoichezea timu ya Taifa ya Ujerumani.
Bahati mbaya kwa Scoltland ilitokea ambapo walijikuta katika dakika za majeruhi wakicheza pungufu baada ya Charlie Mulgrew kuoneshwa kadi nyekundu.
Emotional: Anya seemed to be in disbelief after racing though and side-footing the ball home to score for Scotland against the summer's World Cup winners Germany
Hisia kali: Anya alionekana kutoamini baada ya kuifungia Scotland bao la kuaswazisha dhidi ya mabingwa wa dunia Ujerumani 
Easy does it: Thomas Muller remained composed in the area to side-foot the ball into the roof net to put Germany back in front with twenty minutes remaining
Ukiujua mpira unaweka kiulaini tu: Thomas Muller akifunga bao la pili wakati zikisalia dakika 20 ngoma kumalizikaBack in front: Muller celebrates after restoring Germany's lead just four minutes after Anya's 66th minute leveller
Watu kimyaaa!: Muller akishangilia baada ya kuiokoa Ujerumani kwa kuifungia bao la pili dakika nne tu baada ya Scotland kusawazisha 
Kikosi cha Germany (4-3-3): Neuer 6, Rudy 7, Howedes 7, Boateng 7, Durm 7, Kroos 7, Kramer 7, Gotze 7, Reus 7 (Ginter, 90), Schurrle 6, (Podolski, 84), Muller 8.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Zieler, Grosskreutz, Sam, Rudiger, Gomez, Weidenfeller.
Mfungaji wa mabao: Muller, 18, 70. 
Kadi ya njano: Durm, Muller.
Kocha: Joachim Low, 7.

Kikosi cha Scotland (4-5-1): Marshall 7 Hutton 6, R Martin 6, Whittaker 6, Hanley 6, Mulgrew 6, Morrison 6, D Fletcher 5 (McArthur, 57), Bannan 5 (S Fletcher, 57) Anya 8, Naismith 7.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: A McGregor, Greer, Maloney, Bryson, McDonald, Burke, Reynolds, Forsyth, C Martin, Gordon.
Kadi ya njano: Hanley. 
Kadi nyekundu: Mulgrew. 
Kocha: Gordon Strachan, 6. 
Mfungaji wa goli: Anya, 66. 
Mwamuzi: Svein Oddvar Moen (Norway), 6.
Mchezaji bora wa mechi: Thomas Muller   
Watazamaji: 65,000 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.