URAIS 2015 SINA MPANGO ASEMA WAZIRI NKAMIA

GEDSC DIGITAL CAMERANaibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni   Mbunge wa Kondoa Kusini ,akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu njiro ambapo alisema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015
GEDSC DIGITAL CAMERABaadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa wanafanya mahojiano na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia leo jijini Arusha katika studio za redio 5 
GEDSC DIGITAL CAMERAMkurugenzi wa Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis akiwa anamsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia wakati akizungumza na waandishi wa habari kulia ni mwandishi wa chanel Ten Jamilah Omary 
GEDSC DIGITAL CAMERAMtangazaji wa redio 5 Mwangaza Jumanne akifanya mahojiano live na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia
GEDSC DIGITAL CAMERAKulia Mwanaisha Suleiman akiwa anafanya yake ndani ya studio za redio 5 mara Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia alipofanya ziara kituoni hapo
GEDSC DIGITAL CAMERAMuonekano wa studio ya Redio 5 wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akifanyiwa mahojiano hewani na mtangazaji wa kituo hicho Mwangaza Jumanne
GEDSC DIGITAL CAMERAMeneja masoko wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia 
GEDSC DIGITAL CAMERAMkurugenzi  wa Radio 5  Bw Robert Francis akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ofisini kwake mda mfupi kabla ya kuingia studio za redio hiyo
GEDSC DIGITAL CAMERA
Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw.Robert Francis  katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia,kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog Pamela Mollel
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya  ubunge
Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa bado hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015
Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu
”Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana”alisema Nkamia
Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo(Habari picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA