Wabunge wanawake wasisitiza ajenda ya hamsini kwa hamsini kutokakwepeka katika Katiba Mpya ijayo.


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Margareth Sitta akifungua semina ya Wanawake iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana akiwahutubia baadhi ya wanawake na wanaume waliohudhuria semina maalum iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) akichangia mada wakati wa semina ya wanawake iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 ambayo ikihusu iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


Baadhi ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi wakati wa semina hiyo. (Picha zote na Edwin Mujwahuzi)
 
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
Katika juhudi za kuleta usawa wa kijinsia na kuinua hadhi ya wanawake, Serikali imefanya jitihada kubwa katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali katika jitihada hizo
Hayo yamesemwa 13 Septemba, 2014 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana wakati wa semina iliyohusu masuala ya kuwapa nyenzo ama uwezo wananawake waweze kushiriki vizuri katika maeneo mbalimbali yanayowakilisha wanawake huku wakiungwa mkono na wanaume.
Mhe. Chana amesema kuwa baadhi ya watu nchini wamekuwa na dhana tofauti huku wakiona wakipotezewa muda pindi mambo yoyote yanayowahusu wanawake yanapozungumzwa wakisahau kuwa ili taifa liweze kufika mahali pazuri na kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania hakunabudi kulitazama kundi hilo la wanawake ambalo ni muhimu.
Mhe. Chana ameeleza kuwa asilimia 51% ya Watanzania ni wanawake ambao wanachangia nguvu kazi kwa upande wa kilimo kwa asilimia 45 ya pato la Taifa, pia asilimia 25 wako katika ajira iliyo rasmi lakini wengi wako katika sekta isiyo rasmi.
“Asilimia 34% pia ya wanavyuo kutokana na takwimu inaonyesha kwamba ni wanawake, kwahiyo ajenda ya wanawake haikwepeki”, alisema Mhe. Chana.
Akizungumzia kuhusiana na masuala ya mchakato wa kusaka Katiba Mpya, Mhe. Chana amesema kuwa katika majadiliano yanayohusu Katiba, ajenda ya wanawake pia haikwepeki.
Mhe. Chana aliongeza kuwa endapo wanawake nchini watawezeshwa basi taifa zima litakuwa limewezeshwa kwani watu wengi waliopata mafanikio ni kutokana na wanawake kutoa malezi bora katika kulea watoto pindi wanapozaliwa hadi kupata elimu.
Aidha, Mhe. Chana amesisitiza juu ya wanawake kushirikishwa katika vyombo vya maamuzi ili kuongeza hali ya uchumi kwa wanawake, hali ya kijamii ya wanawake na ya kisiasa kwa wanawake hao.
“Lazima tuwepo kwenye vyombo vya maamuzi kwani ndiko tunapopata haki zetu kwani huko pia ndiko tunapoweka bajeti ya serikali kuu, bajeti ya serikali za mitaa, kwahiyo tunaanza na vyombo vya maamuzi”, alisisitiza Mhe. Chana.
Naye Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya amesema kuwa Tanzania ina wanawake wenye sifa, na uwezo na maarifa kwenye maeneo yote kuanzia, udaktari, uhasibu, Wahandisi yakiwemo na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa, ajenda ya kufikia hamsini kwa hamsini kwa wanawake haina mjadala, hivyo wanawake wana haki ya kuhusishwa katika masuala ya ungozi kama ilivyo kwa wanaume.
“Mwanamke kwenye uongozi ni lazima aweze kuliko mwanaume, anatakiwa ajiwekee mikakati yake mwenyewe ya kujihudumia (selfcare) ili kuwa na muda wetu wenyewe”, alisema Bi. Mallya.
Bi. Mallya aliongeza kuwa wanawake wanapaswa kutambua kuwa ajenda inayohusu mapambano ni ajenda ya muda mrefu ndani ya maeneo yao ya uongozi.
Bi Mally alisisitiza kuwa, wanawake wajitahidi kuwa wanasiasa kwenye vyama vya siasa, wawe wabunge pia wawe viongozi kwenye taasisi za umma na binafsi ili kufanikisha suala lao la hamsini kwa hamsini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI