BENKI YA DUNIA NA IMF YAANZA MIKUTANO YA MWAKA MJINI WASHINGTON DC - MAREKANI


 Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi.Mwanaidi  Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula.
 Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na Serikali Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu  masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.

Kila mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.

Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. 

 Mikutano hii inatoa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. 

Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha. Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira. 

 Imetolewa na: 
Ingiahedi Mduma 
Msemaji -Wizara ya Fedha 
Washington D.C 
7/10/2014

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI