ENEO LA SHULE LAUZWA KINYEMELA


MASSHINE BULUDOZAEneo la Shule ya Msingi Magamba ambalo linadaiwa kuuzwa kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara ya Sitalike –Mpanda kwa Kiwango cha lami likichimbwa kifusi.
magamba
Kibao Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Nsimbo 
(Picha na Kibada kibada –Nsimbo Mlele)
Na Kibada Ernest Kibada Mpanda Katavi
SEHEMU ya  eneo la  Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo , Mlele Mkoa wa Katavi limeuzwa kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara  kwa kiwango cha Lami  kutoka Sitalike hadi Mpanda Mjini .
Eneo hilo la shule limeuzwa kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kichina lijulikanayo kwa Jina la Railway  Sevanth Group lenye Makao yake jijini Dar es salaam.
Eneo hilo limenunuliwa  kwa ajili  ya kuchimba kifusi kinachotumika kutengenezea barabara ya lami inayoendelea kujengwa kutoka Kata ya Sitalike hadi Mpanda Mjini.
Akizungumzia kuhusu eneo hilo kuuzwa kwa Mkandarasi huyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi  Magamba Mwl. Yohana Kasansa ameeleza kuwa yeye hatambui kuuzwa kwa eneo hilo  bali anatakumbua kuwani eneo halali la Shule.
 
Akaeleza kuwa yeye anaona tu  shughuli zikiendelea za uchimbaji wa kifusi kwa ajili ya kutengeneza barabara lakini hajui nani alitoa ruhusa.
 
Alisema eneo hilo   la shule hutumika kwa ajili ya kulima mazao aina ya    mahindi kwa ajili  chakula cha shule   kwa watoto. 
 
Mwalimu Kasansa akaongeza kuwa wakati linapokuwa halitumiki kwa ajili ya kilimo huwa linaachwa wazi lakini baada ya kuchimbwa udongo kwa ajili ya kifusi limebaki na mashimo ambayo ni hatari kwa watoto na hasa wakati huu ambao mvua zinapokaribia kunyesha. 
 
 Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Magamba George Pius alipotakiwa kuelezea uuzwaji wa eneo la Shule ambayo ni mali ya Kijiji,  alisema  kuwa hatambui ni nani aliuuza.
 
“Kufuatia hali hiyo niliwaandikia barua ya kuwataka wasitishe shughuli za kuchimba kifusi katika eneo hilo ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lakini hawakutekeleza na waliendelea na kazi kama unavyoona hapo kazi zikiendelea”alisema Pius Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Magamba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.