FILAMU YA MAPENZI YA MUNGU KUINGIA SOKONI LEO

Mwezi, Wiki na Siku zikabaki, Masaa  kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA MUNGU Kuingia Sokoni, Sasa filamu hiyo yaingia sokoni leo ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu hiyo Ni Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana kama Linah Sanga, kwa Kushirikiana na Elizabeth Michael bila Kumsahau Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU...Ni Filamu ambayo Kisa chake na Mafunzo yake yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo kiukweli ina hadhi na vigezo vya kimataifa......

Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na kuthibitisha kuwa kweli Sanaa ni Kazi.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*