GARI LILILOBEBA NG’OMBE LAPATA AJALI UBUNGO DAR

Mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma, akionyesha eneo la bega aliloumia katika ajali. 
Gari lilivyokuwa baada ya ajali.Mifugo ikiwa kando ya barabara baada ya ajali.Eneo ajali ilipotokea. MFANYABIASHARA mmoja wa mifugo (ng’ombe) na dereva waliokuwa katika lori lililokuwa limebeba mifugo hiyo, leo wamenusurika katika ajali iliyotokea asubuhi eneo la Ubungo-Mataa, jijini Dar es Salaam.
Gari hilo lililokuwa limebeba ng’ombe wapatao thelathini likitokea Wilayani Kondoa, Dodoma, limepata ajali na ng’ombe kadhaa kuumia sehemu mbalimbali za miili .
Wakizungumza na mtandao huu, mashuhuda wamesema tukio hilo lilifuatia mwendesha pikipiki (bodaboda) kukatiza kwa kasi mbele ya gari hilo na dereva alipoamua kuwakwepa, gari lilianguka.
Aidha mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma, amelipongeza jeshi la polisi na askari kwa ulinzi walioufanya hapo kwani hakuna kitu kilichopotea

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*