JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR.


 Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai akizindua Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
 Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda akitoa nasaha zake kwa Watendaji hao katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo huko Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View.
 Mkuu wa Kitengo cha Dawa na Vipodozi Zanzibar Bora Lichanda akifafanua Jinsi Kitengo chao kinavyofanya kazi kwenye Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
  Mkuu wa Bodi ya Madawa na sumu Nchini Kenya Dkt. Ronald M. Inyangala akichangia kitu katika mafunzo hayo.
 Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi kutoka Zanzibar Hidaya Juma Hamad akizungumza na Wanahabari nje ya Ukumbi wa Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View ambapo mafunzo hayo ya siku tano yanafanyika.

 Mgeni rasmi Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai (kati kati) waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo-Zanzibar).



Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar  ikiwa ni Mkakati wa kuunda Chombo maalum cha pamoja cha usimamizi na usajili wa Dawa utakaofanywa katika nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanalengo la kuweka Msimamo wa Pamoja na Viwango sawa kwa Bodi za Vyakula na Dawa ili Dawa itakaposajiliwa katika nchi moja ikubalike kimatumizi katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai amesema kuwepo kwa Chombo cha Usimamizi wa Pamoja katika Nchi hizo kutasaidia kuondokana  na Tatizo la Uingizwaji wa Dawa zisizofaa Kimatumizi katika nchi hizo.

Amesema Chombo hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo kwa vile kutakuwa na Mikakati ya kupeana taarifa za karibu kuhusu Dawa zinazosajiliwa na kusambazwa katika nchi zao.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda amesema Malengo ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha Vitengo vyote vya Nchi Wanachama vinajengewa uwezo na Ufanisi ili viwe katika Ubora unaofanana.

Amesema kwa sasa kila nchi inatathmini na kusajili Dawa kivyake na kwamba kukamilika kwa Mafunzo hayo itakuwa ni hatua kubwa ya kufikia Makubalianao ya kuanzishwa kwa Chombo kimoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza pembeni ya Mkutano huo Mratibu mwenza kutoa Zanzibar  Hidaya Juma Hamad amesema kukamilika kwa Chombo hicho kutasaidia sana upatikanaji wa Dawa salama katika nchi husika. Amesema sambamba na hilo kutasaidia kupunguza gharama na matumizi mengi ya rasilimali ambayo yangetumika katika nchi zingine.

“Dawa Moja kuisajili inaweza kuchukua miaka miwili kwa hiyo Dawa hiyo itakaposajiliwa katika nchi moja itakuwa na uhalali wa kutumika katika nchi nyingine bila kusajiliwa tena, na hapo gharama kubwa zitakuwa zimeepukwa” Alisema Hidaya.

Pamoja na Zanzibar kupewa mafunzo hayo bado inakabiliwa na Changamoto nyingi zinazokwaza ufanisi wao ikiwemo uhaba wa Fedha, Ofisi ndogo na Idadi ndogo ya Wataalamu na Watendaji wa kukagua Maduka ya Dawa, Vyakula na upekuzi bandarini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.