KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA ENEO LA TANGANYIKA PAKERS AMBAPO NHC INATEKELEZA MRADI WA YUMBA WA (KAWE CITY)

      

1Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake na  jimbo la Kahama  Mbunge Mh. James Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini,  kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba  la Taifa NHC akielekeza jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi. 3Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,  Mazingira na Maliasili Mh. Hery Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mh. James Lembeli wakimsikililiza 4Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mh. James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka 5Baadhi ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la NHC. 7Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili  na Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la  Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na shirika hilo la NHC. 8Huu ndiyo uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi mahali ambapo sasa panaanzishwa mradi wa nyumba za NHC. 9Waziri wa Ardhi Nyumba  na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo. 10Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  na mbunge wa Kahama  Mh. James Lembeli akishuka kwenye gari katika eneo la Tanganyika Pakers mahali ambapo patatekelezwa mradi wa Kawe City unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC. 12Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu  13Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba  la Taifa NHC akendelea kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika  eneo la Tanganyika Pakers Kawe. 14Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam. 15Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mh. James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo mikubwa ya makazi  , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh.  Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati  hiyo na na Mbunge wa Mafia. 17Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata taarifa ya awali..

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.