KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA AKABIDHI ZAWADI YA BASI DOGO BWAWANI SEKONDARI KATIKA MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA NNE



 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi funguo za Basi dogo kwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga(kushoto). Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi katika ziara mbambali za Mafunzo hivyo kuondoa kero kubwa ya Usafiri shuleni hapo.
 Sehemu ya Wahitimu katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne, Bwawani Sekondari wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
 Kikundi cha Wasanii kinachoundwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari kikijiandaa kutumbuiza mbele ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Shule ya Bwawani Sekondari, Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014, Mkoani Pwani. 

 Mama mzazi wa Mhitimu wa Kidato cha Nne kutoka familia ya Kifugaji ya Kimasai akimbusu mkono Mtoto wake ambaye amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa na Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014 katika Bwalo la Bwawani Sekondari, Mkoani Pwani Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.