KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA ULINZI WA AMANI KWA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA SADC, MKOANI KILIMANJARO

      

imageKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu) akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. image_1Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki kikamilifu Mafunzo hayo. image_2Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah. image_3Wakufunzi wa Mafunzo hayo wakisikiliza hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC. Jumla ya Wahitimu 27 toka Nchi za SADC wameshiriki Mafunzo hayo kikamilifu katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa kwanza kulia) ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Kanali Sambulo Ndlovu toka Zimbabwe(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart(wa tatu kushoto) ni Mkufunzi toka Tanzania, Ahmad Mwidadi(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Zambia, Mrakibu wa Polisi Nchini Zambia, Edward Njovu. image_4Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. image_5Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa sita kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. image_6Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(katikati) ni Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo toka Nchini Tanzania, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Pendo Kazumba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI