KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO WA KUHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WADOGO HUSUSANI WANAWAKE.

Meneja wa Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika kampeni ya GROW 
 
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye mfano wa Kuigwa
Mshindi wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.
Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.
Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Balozi wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi.
Wa kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.