KATIBA INAYOPENDEKEZWA YAOMBEWA DUWA NJEMA


PIX 1.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wakati wa dua ya kuiombea Katiba mpya Inayopendekezwa
PIX 2.PIX 5.
Viongozi wa Dini toka wadhehebu ya Kiislamu, Kikristo, Wasabato, Wahamadiya, Jamaat Khan, Singh Temple pamoja na CCT-Dodoma wakiongoza dua zao leo mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
 
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
 
DUA ya shukurani ya kuiombea Katiba mpya Inayopendekezwa imefanyika jana mjini Dodoma na viongozi mbalimbali wa dini toka madhehebu mbalimbai yakiwemo ya Kiislamu, Kikristo, Wasabato, Wahamadiya, Jamaat Khan, Singh Temple na CCT-Dodoma.
 
Akiongea wakati wa dua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi alisema kuwa katika mchakato mzima wa kusaka katiba mpya, shughuli mbaoimbali za maendeleo zikiwemo shughuli za kibiashara, shughuli za kibenki, wanafunzi na shughuli nyingine za kiofisi ziliweza kuendelea kama kawaida pasipo shari yoyote hadimchakato wa kuipata Katiba ulipofikia.
 
Dkt. Nchimbi alieleza kuwa, kuna watu waliotumia muda wao mwingi katika kuhakikisha kuwa mchakato unafikia lengo kwa kukesha usiku na kufanya dua maalum ya kuiombea katiba hiyo ili iweze kupatikana na aliongeza kuwa wapo waliofanya kazi kubwa kwa kukesha huku wakifanya kazi ndani ya Bunge Maalum kwa ajili ya kufanikisha  mchakato huo.
 
“Kipindi hiki cha mchakato wa Katiba, Watanzania na marafiki zetu tumeongea na Mungu kwa namna isiyo ya kawaida, tumekutana hapa kukiri kwa maana tulimuita Mungu naye ametuitikia, hakika  yeye ndiye aliyetufanya kuipata Katiba hii”, alisema Mhe. Nchimbi.
 
Nao Viongozi wa dini mbalimbali walipata wasaa wa kutoa dua zao kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuiombea nchi amani pamoja na Katiba yenyewe kwani itakuwa mkombozi kwa Watanzania.
 
Akiongea kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Dodoma, Mhe. Balozi Job Lusinde alisema kuwa ni jambo la busara kuomba dua kwa Mungu kuhusu mchakato wa kupata Katiba na pia ni wasaa wa kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha wale wote waliojitolea kufanikisha kuipata Katiba hiyo.
 
Aidha, alisema kuwa tangu Dkt. Nchimbi awe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, watu wameshuhudia msimamo wake kuhusu umuhimu wa umoja, upendo, mshikamano kwa wananchi wote wa Dodoma kwani ameweza kuzishirikisha dini zote, na kuwaunganisha, pia amekuwa wa kwanza katika kuutukuza mji wa huo wa Dodoma.
 
“Ndugu zangu wananchi wa Dodoma, tumshukuru RC wetu wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kutupa muda wa dua kama hii ya leo”, alisema Balozi Lusinde.
 
Mchakato wa Katiba mpya unatarajiwa kufikia hatua nyingine hapo kesho ambapo Marais toka Tanzania Bara na Zanzibar, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein watakabidhiwa Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba mwaka huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI