Staa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ .Kudhihirisha kwamba wameshibana,
kuna wakati KAMA walivyo Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel kwa sasa
ndivyo walivyokuwa Wema na Kajala Masanja miezi kadhaa iliyopita.Wema na
Kajala walikuwa mashosti wa kufa mtu, walishibana na kupeana siri zao
zote hususan zile za ndani kabisa. Wema aliamua kujitolea Sh. Mil 13
kulipa faini ambayo ilimnusuru Kajala kuswekwa gerezani.Baadaye walikuja
kutofautiana, kila mtu akaishi kivyake. Yakazungumzwa mengi
kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi ni kupishana kauli kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza kutofautiana na kupatana.
kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi ni kupishana kauli kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza kutofautiana na kupatana.
Kwa
upande wao suala la kupatana limekuwa zito, ugomvi wao haufiki tamati
hukukila kukicha ni malumbano ambayo yanawagawa mashabiki.
Mastaa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel wakipozi.Tatizo
kubwa linalochagiza ugomvi wao ni mitandao ya kijamii, kumezuka makundi
ambayo yamekuwa yakitumia utabiri wao wanaoufahamu wenyewe kuzidi
kuchochea ugomvi uliokuwepo kati ya mastaa hawa wawili na wengine
wakitumia matusi mpaka ya nguoni kutukana wa upande wa Wema na Kajala.
Makundi
hayo ndiyo yamekuwa chachu kubwa ya bifu lao na kuzidisha mapambano kati
ya mastaa hawa ambao naamini wanapendana sana, sitaki kuamini kabisa
kama Wema hampendi Kajala, na sitaamini kama Kajala hampendi Wema.
Staa
wa filamu Bongo,Kajala Masanja.Ndiyo maana siku ambayo walipatana na
kuzungumza kwa muda nyumbani kwa msanii Aunt Ezekiel, mastaa hao
walipata fursa ya kukaa pamoja na kuzungumza baada ya ugomvi wao kila
mmoja alitoa chozi kuonyesha jinsi gani kila mmoja anaumia anapokuwa
mbali na mwenzake.
“Mimi
nilikuwa napenda sana kukuangalia wewe na siyo timu zinazotuzunguka
zinazidi kututia chumvi tugombane, nakupenda na ninajua ni rafiki mwema
kwangu lakini unasikiliza sana maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala
niliyosikia akimwambia Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
Mastaa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja
katika picha ya pamojaManeno hayo waliyoambizana huku kila mmoja akitoa
machozi, yalisahaulika kwa siku tatu tu kwani viliibuka vitu ambavyo
havikujulikana vilipotokea na kuanzisha ugomvi mwingine mpya na
kuwafanya wawili hawa kuvurugana tena kwa kasi mpya na nguvu mpya.
Nathubutu
kusema kwamba ugomvi wa mastaa hawa mara nyingi unachagizwa na mitandao
ya kijamii. Hizi zinazojiita Team Wema na Team Kajala ndiyo tatizo
kubwa.Nasema ni tatizo kwa sababu hata ukiangalia kwa makini, kipindi
cha nyuma mastaa hawa walipokuwa wanaanzisha urafiki wao, timu hizo
hazikuwepo ndiyo maana waliweza kudumu.
Kwa nini
wanakubali kutawaliwa na hizi Team? Kwa nini waruhusu maisha yao ya kila
siku yaingiliwe uhuru wao wa kufanya mambo yao? Si sawa!
Mimi
naamini kabisa kama mastaa hawa wangekuwa na ugomvi wao bila hizi Team
kuingilia kati wangeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao mapema
sana lakini tatizo kuna watu wa pembeni wenye kuzoa maneno huku na
kupeleka kule.
Kwa jinsi
ninavyoona mimi, hizi Team zikiendelea hivi na kwa mastaa wengine, ipo
siku watasababisha hata mauaji kwa jambo ambalo halina kichwa wala
miguu. Niwasihi Kajala na Wema wasijisahau kuwa wao ni biashara,
mashabiki wengi wanapenda kuona kazi zao, wangeweka tofauti zao pembeni
wafanye kazi na washirikiane hata kutengeneza filamu ya pamoja.
Naamini
wakiweka pembeni hizi Team, wakaacha kusikiliza maneno ya kinafiki
yanayoundwa na baadhi ya wasanii wasiopenda urafiki wao, basi wataishi
vizuri na watafanya kazi zao pamoja!
Comments