KINANA ASHIRIKI UPANDAJI MAHINDI MUHEZA,TANGA


Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mahindi katika shamba la mfano katika Kijiji cha Kwemnyefu, wilayani Muheza, Tanga wakati wa ziara ya kuiamarisha uhai wa chama na kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (katikati), akishiriki kupanda mahindi katika shamba la mfano katika Kijiji cha Kwemnyefu, wilayani Muheza, Tanga wakati wa ziara ya kuiamarisha uhai wa chama na kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kinana akiungana na wanachi kuchimba mashimo ya kupandia mahindi katika shamba la mfano katika Kijiji cha Kwemnyefu, Muheza mkoani Tanga.
Kinana na Nape wakiwa na baadhi ya wananchi na majembe begani baada ya kushiriki kupanda mahindi  katika shamba la mfano, katika Kijiji cha Kwemnyefu, wilayani Muheza, Tanga.
Kinana akilakiwa na wananchi wa Kata ya Kilulu alipokwenda kushiriki ujenzi wa tawi la CCM katika Kijiji cha Kilulu,
Mmoja wa wanachama wapya wa CCM, akipokea kadi baada ya kujiunga nachama hicho katika mkutano uliofanyika mjini Muheza.
Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kilulu.
Kinana akizungumza baada ya kukagua Kituo cha Habari za Kilimo Songa
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya  cha Ubwari kinachokarabatiwa na kuwekewa samani.
Kinana akikagua majengo ya Kituo cha Afya cha Ubwari wakati wa ziara yake mkoani Tanga


Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Muheza

Mkazi wa Muheza, Abdulrahman Kigwe ambaye ni wajina wa Katiibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiuliza maswali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*