KINANA ATINGA JIMBO LA ISIMANI,IRINGA NA KUWATAKA VIONGOZI KUWATUMIKIA WANANCHI IPASAVYO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani,  William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo
 Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.
 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CC,
 Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM
 Wanachama wa CCM Shina namba 6 katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya wakicheza kwa furaha wakati Kinna alipofika kuzungumza nao
 Kinana akizungumza na wananchama wa shina hilo. Kulia kwake ni Balozi wa shina hilo Chengula Mlula
 Kinana na Lukuvi wakitoka kukagua ujenzi wa Zahanati ya Magozi Kata ya Ilolo Mpya, Isimani
 Kinana na Lukuvi wakijadiliana jambo baada ya kukagua ujenzi huo

 Wamasai wakiingia kwenye mkutano kutumbiza kwa ngoma ya asili

 Wasanii wakicheza ngoma ya asili ya kabila la wasukuma


 Lukuvi akimkabidhi kompyuta na mashine ya kudurufia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pawaga Charles Mgimwa kwa ajili ya matumizi ya shule
 Mgimwa akifurahia msaada huo
 Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo, Shakila Kiwanga wakati wa mkutano huo
 Mbunge wa Jimbo la Isimani, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akielezea miradi inayyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.
 Mmoja wa wananchi akiuliza swali kwa Katibu Mkuu Kinana kuhusu mgogoro wa ardhi  wa wanakijiji na Jeshi la Magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk. Beatrice  Ishengoma akijibu swali hilo ambapo alisema kuwa kwa asilimia kubwa wamelitafutia ufumbuzi na kwamba kilichobaki ni wizara husika kwenda kupima na kuweka alama za mipaka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.