KIMBUNGA CHA KINANA CHAWAKUMBA KATIBU WA CHADEMA NA WAFUASI WAKE 26 NYOLOLO,MUFINDI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionesha kadi 27 za wananchama wa Chadema  waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM kaatika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Nyololo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010. Kulia aliyevaa shati jeupe ni aliyekuwa Katibu wa Kata ya Igowole, Josephat Soda ambapo wengine ni miongoni mwa walio kuwa wafuasi wa Chadema.
 Aliyekuwa Katibu wa Chadema Kata ya Igowole, Joephat Soda akikabidhi bendera ya chama hicho kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya yeye na wenzie 26 kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
 Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Josephat Soda baada ya kutanga kujiunga na CCM katika mkutano huo.
 Josephat Soda akielezea jinsi alivyoamua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ambapo alisema amechoka na chama kilichosheheni uongo, ambapo viongozi wa Chadema alidai kuwa walitoa maagizo kuwaakope fedha za  kujengea Mnara wa mwandishi wa habari Marehemu David Mwangosi, aliyeuawa wakati wa vurugu za Chadema na Polisi katika Mji wa Nyololo, ambapo walimuahidi kumtumia fedha zilizotumika kujenga mnara huo ahadi ambayo hadi sasa haalipwa na anadaiwa na muuza simenti na muuza saruji alikokopa. CCM imeamua kulipa madeni yote aliyokuwa akidaiwa.
Wanachama wa CCM wakiwemo wapya kutoka Chadema, wakiapa kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi wakati wa mkutano huo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI