Ludewa kung'ara kwa umeme


   

IMG-20141026-WA0010_9f6a2.jpg
Mbunge Deo Filikunjombe
IMG-20141026-WA0008_cf7fb.jpg
Wananchi walishirikiana kwa kiasi kikubwa sana
IMG-20141026-WA0007_ba072.jpg
Kazi ilianzia mbali sana mpaka kuupata umeme. (P.T)
IMG-20141026-WA0006_23af0.jpg
Kule Ludewa, wiki hii imekuwa ni juma la furaha pomoni; Ilikuwa kwanza ni wiki ya furaha kubwa sana - kwangu mimi mwenyewe binafsi, na pili ilikuwa ni furaha kubwa - kwa wapiga kura wangu na wale wote wanaoitakia mema wilaya yetu ya Ludewa.
Nilikwenda katika Vijiji vya Mlangali na Mkiu kuwajulisha kuwa zile jitihada zangu mie mbunge wao za kuwaletea nuru ya matumaini zimezidi kubarikiwa zaidi na zaidi.
Nilikwenda Mlangali kuwajulisha kuwa, tukishirikiana na Baba Askofu Alfred Maluma wa Kanisa Katoliki la Jimbo la Njombe, nimepata fedha kwaajili ya kuwapelekea umeme katika kijiji cha Mlangali. Na vile vile katika kijiji cha Mkiu.
Nilipomaliza mkutano wa hadhara pale Mlangali, wananchi wa Mlangali waligawanyika katika makundi makundi; wananchi wengine walirukaruka juu kwa furaha na wengine walibaki wameketi chini wakiwa wameduwaa. Hawaamini masikio yao.
Ni kweli. Baba Askofu Maluma, akishirikiana na ACCRA - wale waliojenga umeme wa Lupande, Mawengi na Madunda - wapo tayari kupeleka umeme katika vijiji 20 zaidi, kwa gharama ya Tshs. 14 bilioni, ufadhili wa Benki Ya Dunia.
Nikiwa Mlangali, nimewataka wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa watekelezaji wa mradi, kwa mfano, nimewataka wasidai fidia katika maeneo yatakayoathirika na njia za umeme, etc Na wamekubali.
Utekelezaji wa mradi huu unaanza juma hiki October 28, 2014.
Vijiji vitakavyopata umeme chini ya mradi huu wa sasa ni pamoja na vijiji vya: Lugarawa, Mkiu, Mlangali, Itundu, Lufumbu, Luvuyo, Ligumbiro, Utilili, Lupanga, Lusala, Masimbwe, Madope, Mangalanyene, Manga, Madilu, Ilawa, Mfalasi, Mdilidili, Ilininda na Kijiji cha Kiyombo.
Ilikuwa pia ni habari njema kwa sababu, nimepata fedha kwaajili ya kupeleka umeme wa gridi ya taifa katika vijiji vya: Mavanga, Mbugani, Mundindi, Amani, Shaurimoyo, Mkongobaki, Madindo, Ludende, Ugera, Lipangara, Maholongw'a, Ibumi, Masimavalafu, na Nyamalamba.
Ikumbukwe kuwa sasa hivi tunashirikiana na wananchi na shirika la TANESCO na REA kupeleka umeme katika Vijiji vya Nindi, Ntumbati, Lupingu na Kilondo.
Na kwamba pia, TANESCO wamekubali kupeleka umeme katika vijiji 14 vya tarafa yote ya Masasi ambavyo ni vijiji vya:- Kimerembe, Ngalawale, Nkomangombe, Kipangala, Lifua, Luilo, Lihagule, Masasi, Usagalu, Nsungu (Manda), Igalu, Mbongo, Ilela, Ngerenge na Kijiji cha Kipingu.
Deo Filikunjombe,
Mbunge wa Ludewa (CCM).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.