LUNDENGA AKANUSHA MISS TANZANIA KUJIUZULU


HMB_3760
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
misstz1
Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU