MHITIMU WA CHUO AVUA NGUO ZOTE JUKWAANI ALIPOITWA KUPEWA CHETI ZA KUMALIZA CHUO


Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na boxer.

Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa.

Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi.

Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU