NMB YATOA SHILINGI MILIONI 19.4 KUDHAMINI MASHINDANO YA GOLF YATAKAYOFANYIKA OKTOBA 11-12 2014


Mkuu wa Kitengo cha Wateja na Makampuni Makubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.
Rais wa Chama cha Gofu Tanzania, Joseph Tango. 
Mkuu wa Kitengo cha Wateja na Makampuni Makubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto), akizungumza katika
mkutano huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko na Matukio wa Benki ya NMB, Josephine Kulwa, 
Rais wa Chama cha Gofu Tanzania, Joseph Tango na Makamu Naodha wa timu ya gofu Tanzania, Shakil Jaffer. 
Mkuu wa Kitengo cha Wateja na Makampuni Makubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 19.4, Rais wa Chama cha Gofu Tanzania, Joseph Tango (kulia), kwa ajili ya kudhamini mashindano ya mchezo wa gofu ya Nyerere Masters yatakayofanyika Oktoba 11 na 12 mwaka huu viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kumbukumbu ya miaka 15 ya Mwalimu Julius Nyerere. Katikati ni Makamu Naodha wa timu ya gofu Tanzania, Shakil Jaffer. 
Makamu Naodha wa timu ya gofu Tanzania, Shakil Jaffer (kulia), akizungumza katika mkutano huo. 
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa NMB, Doris naye alikuwepo
katika hafla hiyo.



Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB imetoa sh.milioni 19.4 kwa ajili ya udhami wa mashindano ya mchezo wa gofu yatakayofanyika kuanzia Oktoba 11-12 mwaka huu katika viwanja vya Klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam.


Akiuzungumzia udhamini huo Dar es Salaam leo Mkuu wa Kitengo cha Wateja na Makampuni Makubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi  alisema wametoa udhamini huo ili kuendeleza mchezo wa gofu nakushukuru taasisi ya gofu kwa kuona umuhimu yakuishirikisha benki hiyo.

Mashindano hayo ya gofu yatakayojulikana kama  Nyerere masters yatahusisha wachezaji gofu Tanzania nzima huku zawadi mbalimbali zikitegemewa kutolewa kwa rika zote zitakazoshiriki.
"Tunakishukuru chama cha gofu kwa kutupa heshima ya kuwa wadhamini wao na pia nia muendelezo wa udhamini kwenye michezo".alisema Mponzi.

Aidha alielezea udhamini mbalimbali unaofanywa na benki hiyo katika kuendeleza michezo Tanzania.


Wakati huo huo,mwenyekiti wa chama cha gofu,Pauk Mathisen aliishuru benki hiyo kwa udhamini huo kwa miaka mitatu mfululizo na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kuangalia mashindayo hayo yatayofanyika kwa siku mbili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.