PICHA ZA TUKIO LA MSANII CHIDI BENZI AKIPELEKWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA.

 

 Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
 Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.

Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.

Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.

Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU