PSPF YAENDESHA SEMINA KWA WAJUMBE WA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU TANZANIA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika mkoani Morogoro leo Alhamisi Oktoba 23, 2014
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu(Katikati) na viongozi wengine wa juu wa Mfuko huo na wale kutoka idara ya utumishi wa walimu nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina
 Mtaalamu wa tathmini  wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, James Tenga, akitoa mada kwenye semina hiyo akielezea jinsi tathmini ya mafao inavyofanyika
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Katikati), akiwasili kwenye ukumbi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara, iliyofanyika mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ni muendelezo wa Mfuko, kutoa elimu kwa wanachama wake kutoka makundi mbalimbali. (Picha na Mpiga Picha wetu)
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akisalimiana na Hafsa Mrisho, Mkurugenzi wa Utawala na  Rasilimali watu Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya askari polisi na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa ya Tanzania bara wanaohudhuria semina iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro jana. Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul. (Picha na Mpiga Picha wetu)
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika mkoani Morogoro leo Alhamisi Oktoba 23, 2014
 Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro Alhamisi Oktoba 23, 2014

 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Constatina Martin, akiimba sambamba na Msanii Mrisho Mpoto almaarufu kama Mjomba, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo Jumatano Oktoba 22, 2014, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF mkoani Morogoro
 Mfanyakazi wa hoteli, akijaza fomu za kujiunga na mpango wauchangiaji wa hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, pembezoni mwa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu mkoani Morogoro

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba 22, 2014, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba 23, 2014.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, akiwasalimia wajumbe wa semina wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF
 Mjumbe wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, akisoma kipeperushi chenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na mfuko huo, wakati wa semina hiyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI