Viongozi wa CCM wapewa mafunzo ya Uchaguzi

                          


IMG-20141024-WA0001_c769f.jpg
Hii ni Pikipiki aliyokabidhiwa katibu kata ikiwa ni zawadi iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Makungu kwa ajili ya kuwafikia wanachama kwa haraka wakati wa utendaji wa kazi za chama.
IMG-20141024-WA0002_a2bb7.jpg
Mtaturu alikabidhi baiskeli sita kwa makatibu tawi kwa ajili ya kuwafikia wanachama kwa haraka wakati wa utendaji wa kazi za chama.
IMG-20141024-WA0003_36091.jpg
Mtaturu akizungumza jambo Picha na Mathias Canal(P.T)
IMG-20141024-WA0004_68c31.jpg
Na Mathias Canal
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza ziara ya mafunzo kwa viongozi wa chama hicho kwa ajili ya kuhamasisha na kujijenga katika kuwapata viongozi watakaogombea uchaguzi wa serikali za mitaa kuanzia ngazi ya shina, tawi, hadi kata kupitia tiketi ya chama hicho.
Kwa upande wa Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa mafunzo hayo yalianza tarehe 20/10/2014 na kumalizika tarehe 24/10/2014, huku CCM ikiamini kuwa vyama vya upinzani vimepoteza muelekeo hivyo haviwezi kuambulia kitingoji wala kijiji.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kijijini Mabaoni Kata ya Makungu,Wilayani humo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu amesema kuwa Wilaya hiyo ina jumla ya vijiji 148, vitongoji 605, ambapo wamewatembelea viongozi wote na kuwapa mafunzo na mbinu mbalimbali za ushindi.
Sambamba na hayo Mtaturu alikabidhi baiskeli sita kwa makatibu tawi na pikipiki moja kwa katibu kata ikiwa ni zawadi iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Makungu kwa ajili ya kuwafikia wanachama kwa haraka wakati wa utendaji wa kazi za chama.
Hata hivyo makatibu kata wa CCM Wilayani humo wamempongeza diwani huyo kwa kuwarahisishia kazi ya kuimarisha na kukuza chama kwenye kata hiyo huku wakimuhakikishia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba 14 mwaka huu.
Kwa upande wake Yohanes Kaguo ambaye ni diwani wa kata ya Makungu alisema kuwa vifaa hivyo alivyo vitoa ni maalumu kwa ajili ya kazi za chama na sio kwa matumizi binafsi, hivyo shime kila kiongozi kuzitumia na kuhakikisha ushindi unapatikana Wilayani humo kwani wananchi wana imani kubwa na CCM.
Kaguo alitoa wito kwa viongozi kutofikiria nafsi zao badala yake kuwatumikia wananchi walioipa dhamana CCM tangu kuanzishwa kwa chama hicho, huku akiwasihi wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi kwa kuwa ndiyo haki ya kupiga kura.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI