AZIMIO LA ARUSHA LA KUKABILI UJANGILI LAPITA

      

IMG_5047Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu ulioshirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali uliomalizika jana jijini Arusha na kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Kushoto Mwenyekiti wa mkutano wa kikanda wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha na kulia ni Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli.
Na mwandishi wetu, Arusha
JUMUIYA ya kimataifa imepitisha Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama.
Azimio hilo limepitishwa baada ya mkutano wa siku mbili ambapo pia imekubalika kwamba hali ya baadae ya wanyama barani Afrika ni suala linalohitaji uwajibikaji wa pamoja.
Aidha nchi za Afrika zimetakiwa kuukomesha ujangili na kufanya juhudi ya kuhakikisha wanyama walio katika hatari ya kutoweka wanalindwa na kuhakikisha kundi hilo linakua.
Wanyamama ambao kwa sasa wapo hatarini kutoweka ni tembo, faru na simba.
Mkutano huo uliojumuisha mataifa mbalimbali ya Afrika na jumuiya za kimataifa na kufunguliwa na Waziri wa Mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwa niaba ya rais Jakaya Kikwete, umetoa wito kwa mataifa yote kufanyakazi kwa pamoja kukabili ujangili kwa kushirikisha wananchi wanaoishi na kutegemea wanyamapori hao na mapori yenyewe.
IMG_5051Washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu wakijadilina namna ya kuweka nguvu ya pamoja katika kukabiliana na suala la ujangili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, baada ya mkutano ambao uliangalia sheria zilizopo za kulinda mapori na wanyamapori,uhalisia wa mifumo ya ujangili na uhifadhi, washirika wa maendeleo nao walielezea nia zao za kuendelea kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na mapori katika ukanda wa Afrika ikiwamo Tanzania.
Mkutano huo ambao ulishirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali umeelezwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya kustawisha wanyamapori na mapori yanayowahifadhi.
Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Rais Kikwete, Waziri Nyalandu alisema kwamba mataifa yasidharau nguvu ya pamoja katika kukabiliana na ujangili.
Alisema pia kwamba hali ya baadae ya wanyamapori katika bara la Afrika ni wajibu wa kila mtu na kila taifa na mamlaka nyingine ambazo ni wadau.
IMG_5205Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ambapo amesema UN itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.
Alisema Tanzania katika mchango wake imeanzisha mkakati wa kukabiliana na ujangili na kuunda mamlaka ya wanyamapori ili kuwa na uhakika wa kuendeleza masuala yanayohusu hifadhi na changamoto zake kwa kasi na karibu zaidi.
Washiriki wa mkutano huo wa siku mbili walielezea umuhimu wa kulinda mali asili hizo kwa kuwa ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zote.
Akizungumzia umuhimu wa mali asili Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, alisema ujangili na uhalifu mwingine kwa wanyamapori na hifadhi zao ni changamoto kubwa kwa uchumi unaotegemea utalii, mazingira na maendeleo endelevu.
Alisisitiza kwamba suala la uhalifu kwa wanyamapori na mapori yao ni lazima kufanyiwa kazi kitaifa na kimataifa ikiwamo kikanda.
Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia juhudi hizo za kuhifadhi wanyama na mapori kwa kusaidia kutoa elimu na kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili watu wanaoishi jirani na misitu hiyo.
IMG_5219Pichani juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliomalizika jana jijini Arusha.
Alisema Umoja huo utaendelea kusaidia kupeleka elimu ya menejimenti ya wanyamapori na misitu ili wakazi wa maeneo hayo wafaidi raslimali hizo na kuzitunza.
Hata hivyo alizitaka jumuiya za kimataifa na mataifa kushirikiana katika kufanikisha adhma hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya ICCF ambao ni wenyeji wenza wa mkutano huo, Makamu Mwenyekiti Dk Kaush Arha, alisema mkutano huo ulikuwa na manufaa makubwa hasa wito wa kuweka mikakati ya kurejesha makundi ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kama tembo, faru na simba.
Aidha mkutano umekubaliana juu ya masuala kadhaa ambayo yatasaidia Tanzania kuingia makubaliano na majirani zake kuhifadhi wanyamapori.
IMG_5052Naye Mkuu wa balozi za nchi za Jumuiya ya Ulaya nchini Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyochukua kukabiliana na ujangili.
Amesema Jumuiya ya Ulaya ambayo imekuwa mshirika katika kukabilina na ujangili na hifadhi ya wanyama imefurahishwa na mkutano huo kwa kuamini kwamba kunatakiwa kuchukuliwa hatua za kikanda kuweza kunusuru wanyamapori kwa kuchukua hatua za pamoja.
Ameipongeza Tanzania na majirani zake kwa kuchukua hatua madhubuti za kikanda kukabiliana na ujangili na uharibifu wa mazingira na kusema Jumuiya ya Ulaya ipo tayari kusaidia katika juhudi hizo.
IMG_5063
IMG_5094Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia utiliwaji saini wa Azimio hilo.
IMG_5234Wawakilishi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Malawi, Uganda, Mozambique, Tanzania, na Zambia wakisaini Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama kabla ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) kufunga rasmi mkutano huo uliomalizika jana jijini Arusha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI