Dk. Kigwangala ahimiza amani nchini

 
1Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akizungumza na vikundi mbalimbali mbalimbali vya Joging vilivyoshiriki katika tamasha la Mbio za Amani lililoshirikisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za nchi na kupokelewa na mbunge huyo ambye alikuwa mgeni rasmi, Dr. Khamis Kigwangala amewaasa wanasiasa kutoleta siasa za uchochezi hasa katika mchakato mzima wa Katiba mpya ambapo amesema waachwe wananchi wenyewe waisome waielewe na wao wataamua kama wataipigia kura ya Ndiyo au Hapana, mapokezi hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akijitolea damu kwa kitengo cha Damu salama ambacho kikilishiriki sambamba na tamasha hilo kuhamasisha wanamichezo hao ili wajitolee damu katika kuokoa maisha ya wahitaji wa damu. 3Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini. 4Kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT Bw. Dioniz Malinzi na Bw. Jimmy mmoja wa viongozi wa shirikisho la vyama vya Jogging wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika tamasha hilo. 5Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika mazoezi 6Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani. 7Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani. 8Bw.Abdulla Mohamed Mwenyekiti wa Mipango ya Maandalizi ya tamasha hilo akimkabidhi jenzi Mwenyekiti wa Barza la Michezo BMT Bwa Dioniz Malinzi. 9Mdau wa michezo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza na vikundi hivyo. 10 11Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki kuchezo kigoma cha Amani mara baada ya kupokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja. 12Bw. Dioniz Malinzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT akizungumza jambo na vikundi hivyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Tamasha la Mbio za Amani. 13Vikundi hivyo vikifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja. 14Vikundi hivyo vikiimba wimbo wa Taifa.
.......................................................................
Wanasiasa wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala, amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa, waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo.
Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.
Click here to Reply, Reply to all, or Forward 15.41 GB (73%) of 21 GB used Manage ©2014 Google - Terms & Privacy Last account activity: 5 hours ago Details 10 more buku john Show details Conversation opened. 1 unread message.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI