KINANA ATINGA MASASI, ATAKA CCM IENDELEE KUIBANA SERIKALI JUU YA WAFUJAJI WA FEDHA ZA A UMMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji matofali kwa kutumia mashine ya kujengea ofisi ya CCM Wilaya ya Masasi, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akilakiwa katika Kijiji cha Mwena-Ndanda alipoanza ziara katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara
 Komredi Kinana akivishwa skafu na chipukizi ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika Mkoa wa Mtwara
 Wananchi wakiwa wamejipanga kumpokea Komredi Kinana wilayani Masasi, Mtwara
 Kinana akialimiana na akina mama wajane alipotembelea kikundicha Ujasiriamali mjini Masasi
 Meneja wa Kiwanda cha Ubanguaji Korosho cha Perfect Masasi Mtwara, akimuonesha Komredi Kinana jinsi mtambo kiwanda hicho unavyofanya kazi
 Kinana akiangalia mashine za kubangua korosho katika Kiwanda hicho
 
 Kinana akiangalia jinsi korosho zinavyofungashwa kwenye makasha maalumu ya nailoni
 Meneja wa kiwanda hicho akimuonesha Komredi Kinana korosho zilizofungashwa
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Kate Kamba akielezea jinsi alivyoanzisha kiwanda hicho eneo ambalo zamani lilikuwa na reli mjini Masasi. Kiwanda hicho huajiri wafanyakazi 200. Kinana amezitaka halmashauri kuanzisha viwanda vingi kama hicho, ili korosho ziwe zinabanguliwa hapa hapa nchini badala ya kubanguliwa nje ya nchi. Amesema kuwa licha ya kuongeza ajira bali pia itaongeza thamani ya korosho na bei yake.
Kate Kamba akimuonesha Komredi Kinana korosho zilizofungashwa kisasa kiwandani hapo.
Kinana akishiriki ujenzi wa kingo za barabara mjini Masasi
Wana CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Masasi
Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Akwilombe, akiongoza mkutano kwa kuwakaribisha viongozi wa juu wa chama hicho kuhutubia katika mkutano wa hadhara Mjini Masasi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
Wazee wa Kimila wakimsimika Komredi Kinana kuwa mmoja wa wazee wa kimila wa Masasi wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Masasi.
Komredi Kinana akiwa amesimikwa kuwa mmoja wa wazee wa kimila wa Wilaya ya Masasi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU