KINANA AZOA WANACHAMA WAPYA LULUKI KUTOKA UPINZANI JIMBO LA LULINDI, MASASI

 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utii wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Chiungutwa, Jimbo la Lulindi wilayani Masasi, Mtwara leo. Wapinzani waliovihama vyao na kujiunga na CCM katika jimbo hilo ni CUF 182, NLD 76, Chadema 112 na TLP 53. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ndiye aliyewapokea wapinzani na kuwakabidhi kadi za CCM.
 Wananchi wakimlaki kwa nderemo nderemo Katibu Mkuu alipowasili katika Kijiji cha Machombe, Kata ya Marika kushiriki ujenzi wa bwawa la maji wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa kingo za bwawa la maji katika Kijiji cha Machombe, Kata ya Marika, Jimbo la Lulindi, Wilaya ya Masasi, Mtwara kushiriki wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Komredi Kinana akionesha kadi za vyama mbalimbali vya upinzani zilizorudishwa na wafuasi wa vyama hivyo katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Marika Jimbo la Lulindi, Masasi
 Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika, Jimbo la Lulindi, Masasi
 Kinana akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Sinai akitoka kukagua mradi wa maji wa Chiungutwa, Jimbo la Lulindi
 Kikundi cha kwaya kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Chiungutwa, Jimbo la Lulindi, wilayani Masasi,
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Salma Mgeni akielezea katika mkutano wa hadhara kuhusu watu waliokamatwa wakati wa vurugu Januari mwaka huu, wamefikishwa mahakamani ambapo wengine wapo mitaani baada ya kupata haki yao ya dhamana. Pia alielezea kuhusu fidia za walioathirika kwenye vurugu hizo kuwa tayari zimeandaliwa zipo ofisi ya Waziri Mkuu.
 Mbunge wa Jimbo la Lulindi, Jerome Bwanausi akielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi katika jimbo hilo.

 Kinana akionesha baadhi ya kadi walizokabidhi watu waliohama kutoka vyama vya upinzani na kujiunga na CCM katika mkutano huo
 Waliokuwa wanachama wa upinzani wakikabidhi kadi zao kwa Kinana baada ya kutangaza kujiunga na CCM
 Kadi za waliokuwa wananchama wa vyama vya upinzani zikitandazwa jukwaani
 Kinana akiwapongeza wanachama wapya wa CCM kutoka vyama vya upinzani
Kinana na viongozi wengine wa CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho baada ya kuwapokea wapinzani waliovihama vyama vyao katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kata ya Chiungutwa, Jimbo la Lulindi, wilayani Masasi, Mtwara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA