MCHEPUKO HATARI MWALIMU...WACHOMANA VISU, UTUMBO NJE


Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda. 
KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu. 
Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo. 
Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.

Bw. Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini. Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI